Serikali, taasisi na jamii kwa ujumla zimetakiwa kuchukua hatua zitakazotuwezesha kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa ustawi wa vizazi vijavyo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dkt.Anna Henga wakati wa Uzinduzi wa Taarifa ya Athari za Mabadiliko ya Tabia nchi kwenye Haki za Binadamu uliofanyika kwa njia ya Mtandao.
Amesema Ripoti ya mabadiliko ya tabia nchi na athari zake kwenye haki za binadamu imebainisha baadhi ya mambo ambayo yameonekana dhahiri kuathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi yakiwemo masuala ya afya, upatikanaji wa maji safi, mazingira kwa ujumla wake pia kukosekana kwa usawa, kwani wale wanaoteseka zaidi wakati wa shida ya mazingira ni watu walio hatarini (makundi maalumu).
Aidha amesema Haki ambazo zimeonekana zinaathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi ni pamoja na haki za kijamii kama vile haki ya chakula ‚haki ya afya, haki ya elimu, haki ya upatikanaji maji safi na salama, haki ya kuishi mazingira stahiki,haki ya faragha na familia.

Post a Comment