******
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)kimelaani matukio ya uvunjifu wa Haki za binadamu yanayodaiwa kufanywa na Askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori(TAWA) baada ya kuwepo vitendo vya kupigwa na kuuwawa .
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa (LHRC),Anna Henga,wakati akizungumza waandishi wa habari kulaani matukio ya Uvunjifu wa Haki za Binadamu yanayofanywa na Askari wa TANAPA,TAWA,TFS kwa wananchi wanaoishi karibu na Maeneo ya Hifadhi za Taifa na Mapori Tengefu.
Aidha,Henga,amesema mara baada LHRC kupata taarifa juu ya vitendo hivyo ilituma timu ya maofisa wa kituo hicho walibaini kuwepo kwa vitendo vya kupigwa,vitendo vya mauaji,kudhalilishwa,kufukuzwa kwenye maeneo yao na kunyang'anywa mifugo kinyume na sheria.
Hata hivyo,Henga amesema matukio hayo ni miongoni mwa matukio mengi yanayotokea katika jamii za wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya hifadhi ambapo kwa mwaka huu LHRC kwa mwaka huu imepokea matukio manne ambapo ni kinyume na Haki za Binadamu zilizoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 14-16 ya mwaka 1977.

Post a Comment