**********
Wakala wa usamabazaji wa nishati vijijini REA unalenga kutumia kiasi cha shilingi bilioni 3.2 katika mwaka huu fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa majaribio wa usambazaji wa mitungi ya gesi ya kupikia majumbani laki moja yenye uzito wa kilo sita kwenye kaya za vijiji miji Bure nchi nzima .
Yamesemwa hayo jijini Dar es salaam na mkurugenzi wa uendelezaji masoko na Teknolojia kutoka REA ADVERA MWIJAGE katika kikao na wasambazaji wa mitungi ya nishati ya gesi ya majumbani nchini kilicholenga kuwashawishi wasambazaji hao kuchangamkia zabuni ya mradi huo.
Akizugumza Advera amesema kaya zitakazonufaika na mitungi hiyo ni zile zenye uwezo wa kujaza tena nishati ya gesi kwa ajili ya matumizi endelevu ya nishati hiyo.
Kwa upande wao baadhi ya wasambazaji wa nishati ya gesi ya majumbani wamebainisha kuwa mradi huo ni fursa kwao kwani inakqenda kuongeza wigo wa biashara na ajira kwa vijana kupitia wakala
Mradi huo ni sehemu ya jitihada za serikali za kuhakikisha inaongeza idadi ya marumizi ya nishati safi ya kupikia kufikia asilimia 75 nchi nzima ifikapo 2030.


Post a Comment