Licha ya serikali ya Tanzania kuchukua hatua za kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria chini ya asilimia 1 kwa baadhi ya mikoa lakini Mkoa wa Mtwara, Shinyanga pamoja na Kagera imeonesha kupanda kwa kiwango cha asilimia 15 hadi 20.
Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Idara ya Afya ya ulinzi wa Mama na mtoto Dkt Ahmad Mohamed wakati wa jukwaa la kujadili hali ya ugonjwa wa Maleria Nchini ambalo limeandaliwa na Taasisi ya Health Ifakara.
Amesema takwimu zimeonesha kuwa vifo vitokanavyo na ugonjwa wa malaria bado vimeendelea huku mkakati wa serikali uliopo ni kupata rasilimali ili kutokomeza ugonjwa huo ifikapo 2030.
Dkt Honorat Masanja ni Mkurugenzi Taasisi ya Health Ifakara, amesema jukwaa hilo limelenga kutoa fursa kwa wadau kujadili na kujua mapambano dhidi ya malaria na kutoka na majibu ya pamoja ya nini kifanyike ili kutokomeza janga hilo.
Kwa upande wake msaidizi wa program ya kumaliza Maleria Zanzibar Safia Mohamed Ally amesema kwa kiasi kikubwa serikali visiwani Zanzibar imefanikiwa kutokomeza ugonjwa huo kutokana na hatua mbalimbali ikiwemo unyunyuziaji dawa Nchi nzima.
Itakumbukwa kuwa mei 12 mwaka huu Balozi wa Tanzania Nchini Cuba Humphrey Polepole aliielekeza wizara ya Afya kutenga bajeti ili kununua dawa zinazozalishwa katika kiwanda cha kuua viuadudu kilichopo Kibaha Mkoani Pwani ili kutokomeza janga la Maleria Nchini.

Post a Comment