**********
Mwenyekiti wa Kamati ya Kuitangaza Tanzania ambaye pia ni Katibu Mkuu-Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi jioni hii akihojiwa na Kipindi cha Jahazi Clouds FM, amesema filamu ya Royal Tour imelipa kwani kwa takwimu za Disemba mwaka jana 2022 kwa watalii wa ndani na nje jumla imefikisha watalii 3.8m kwa mwaka ikilinganishwa na jumla ya watalii chini ya milioni 2 mwaka 2021. Lengo kwa nwaka 2025 ni watalii milioni 5.


Post a Comment