TRA: ATAKAYE BAINIKA KUTOA RISITI FEKI FAINI Mil.30


***********
Timothy Marko 

Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imewataka wauza bidhaa na watoa huduma kuhakikisha wanatoa risiti pindi wanapo uza bidhaa au kutoa huduma kwa kutumia mashine za kieletroniki za EFD.

Akizungumza na waandishi Habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipa kodi Richard kayombo mfanyabishara au Mtoa huduma atakayebainika anatoa risiti feki atatozwa faini yashilingi 150,0000 hadi shilingi30,00000.

" Wafanyabiashara na watoa huduma wahakikishe wanatoa risiti kulingana uthamani wa bidhaa sambamba natarehe yamauzo ya bidhaa pamoja na kiasi cha bidhaa ikionesha pia TIN namba ya Manunuzi ".Alisema Richard kayombo. 

Mkurugenzi Kayombo alisema mamlaka hiyo itamchukulia hatua mfanyabishara atakayebainika kutoa risiti feki.

0/Post a Comment/Comments