TRUMP AMHAKIKISHIA RC GEITA UCHUMI KUPANDA.

Mkuu wa mkoa wa Geita,Marthine Shigela,akizungumza na wananchi wa kata ya Nyamirembe.
Mkuu wa Idara ya utekelezaji wa bandari (TPA) ziwa viktoria,Fransisco Mwanga, akitoa maelezo ya kukamilika kwa ukarabati na ujenzi wa bandari ya Nyamirembe.
 Mwonekano wa gati la kutia nanga meli zitakazo hudumiwa na bandari ya
Diwani wa Kata ya Nyamirembe,Nashiru Manampa(Trump) akitoa maelezo mbele ya mkuu wa mkoa wa Geita.
                 ****************

Na Daniel Limbe,Chato

DIWANI wa Kata ya Nyamirembe wilayani Chato mkoani Geita,Bashiru Manampa,maalufu kwa jina la "Trump" amemhakikishia mkuu wa mkoa huo kuwa iwapo bandari ya Nyamirembe itaanza kazi rasmi mwaka huu,uchumi wa mkoa wa Geita utapaa haraka zaidi.

Ni kutokana na wananchi wengi wakiwemo wakulima kutumia fursa za kibiashara kuuza na kusafirisha mazao yao kwenda jijini Mwanza pamoja na nchi jirani za Burundi,Rwanda na Uganda.

"Kama bandari hii itafunguliwa meli ikaja hapa, mheshimiwa mkuu wa mkoa nakuhakikishia baada ya miezi miwili njoo ututembelee utashangaa maana polisi watalazimika kukaa hapa kuzuia watu kutokana na wingi wa abiria...kabla ya meli kusimama kufanya kazi wananchi tulikuwa tunalima,ufuta,mahindi,viazi na mpunga halafu tunasafirisha kwenda mwanza kuuza kwa bei kubwa zaidi" amesema Trump.

Mkuu wa wilaya ya Chato, Deusdedith Katwale,amesema iwapo bandari hiyo italejesha usafiri wa meli kama ilivyokuwa awali, upo uwezekano mkubwa sana wa kuifungua wilaya hiyo ki uchumi na kimaendeleo kwa kuwa itawahudumia wananchi wa wilaya ya Chato,Biharamulo,Ngara,Kakonko na Muleba ikiwa ni pamoja na nchi jirani.

Katwale amesema bandari hiyo ni mradi mkakati kwenye wilaya ya Chato,na kwamba wananchi wanasubiri kwa hamu kubwa kuanza kazi kwa bandari hiyo baada ya ukarabati na ujenzi wake kukamilika kwa aslimia 100.

Akiwa eneo la bandari ya Nyamirembe,Mkuu wa mkoa wa Geita,Marthine Shigela,amesema kutokana na maelekezo aliyopewa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan,ni kwamba bandari hiyo sasa inapaswa kuanza kazi mara moja kwa kuwa tayali ujenzi wake umekamilika tangu miaka miaka mitatu iliyopita.

Ametumia fursa hiyo kuwataka wamiliki wa meli nchini,kuanza kutumia bandari ya nyamirembe kusafirisha abiria na shehena ya mizigo kwa lengo la kuihudumia jamii, ikiwemo kuimalisha uhusiano wa kibiashara kwa nchi wanachama wa afrika mashariki (EAC).

"Bandari hii ni mhimili mkubwa sana wa uchumi katika wilaya ya Chato na mkoa wa Geita kwa ukumla...tunawaalika wafanyabiashara kutoka nchi wanachama wa jumuia ya afrika mashariki kuja kuchukulia mizigo yao kwenye bandari hii hasa nchi ya Burundi,Rwanda,Uganda na Sudan" amesema Shigela.

Hata hivyo amewasisitiza wananchi kutumia fursa hiyo kuzalisha mazao mengi ya chakula na biashara ili wapate tija kiuchumi kwa kuwa watapata bei nzuri kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa ukilinganisha na hali ilivyo sasa.

Awali Mkuu wa idara ya utekelezaji wa bandari (TPA) ziwa viktoria,Fransisco Mwanga,amesema jitihada za kuongea na wenye meli kubwa nchini zinafanyika ili kurejesha safari kwenye bandari ya Nyamirembe ikiwa ni pamoja na kuwapa msamaha wa kulipa kodi ya kutunza mizigo kutoka siku saba za awali hadi siku 30 bure.

                        Mwisho.

0/Post a Comment/Comments