TUCTA:YAIOMBA SERIKALI KUANGALIA KWA UPYA VIWANGO VYA KODI.

                                   *******
Timothy Marko 

Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tucta limeiomba serikali kutazama kwa upya viwango vya kodi na Mishahara katika sekta ya umma na binafsi ili kuweza kuboresha Masilahi kwa Mfanyakazi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam mapema leo  Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA) Said Wamba amesema kuwa nivyema serikali ikaboresha Viwango vyakodi kwa wafanyakazi wa umma sambamba na Mikataba ilikuboresha halibora kwa Mfanyakazi wa Umma.

"Tunaiomba Serikali ifanyie Marekebisho ya Bima ya Afya ili kuweza kumnufaisha Mfanyakazi kwasektavyaumma bila kuumia"Alisema Said Wamba

Naibu Katibu Mkuu Said Wamba alisema kuwa nivyema serikali kujenga utamaduni wa kutana na vyama vya wafanyakazi ilkuweza kujadili Mara kwa Mara changamoto za wafanyakazi nakuzitafutia ufumbuzi.

Alisema Nivyema wafanyakazi katika sekta yaumma kuendelea kufanyakazi kwa ufanisi zaidi natija ilikuweza kuishawishi serikali kufanya Marekebisho hayo ya Mishahara na kodi.

"Wito kwa wafanyakazi wote nchini kuongeza tija katika kazi ilikuweza kupata Nguvu  ya kudai Nyongeza ya Mishahara "Aliongeza Said Wamba. 

Wamba alisisitiza kuwa Nivyema Watumishi wa  uuma kuzingatia Muda wa wakazi uendane sambamba na jasho Lao.

0/Post a Comment/Comments