UMOJA WA MACHIFU KUCHANGIA MILIONI 300 MATIBABU SARATANI.


Timothy Marko. 
TAASISI ya Saratani ya Ocen   Road (OCRI) nchini kwa kushirikiana na umoja wa machifu imeandaa mashindano ya mpira wa miguu kati ya wabunge na Machifu ilikuweza kuhamasisha uchangiaji wa Gharama za matibabu ya saratani nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wah Taasisi ya Saratani ya Ocen Road Julias Mwesilage amesema kuwa Gharama za matibabu ya Saratani kwa Mgonjwa  mmoja nishilingi Milioni 35 ,hivyo kwakushirikiana na umoja wa machifu nchini wameanzishashindano la Mchezo mpira Mei27 kwenye uwanja wa Jamuhuri jijini Dodoma ambapo programu hiyo inalenga kukusanya Shilingi miioni 300.

"Fedha hizi zinalenga  kugharamia huduma ya uchunguzi na tiba ya ugonjwa wa saratani".Alisema Julias
 Mwesilage.

Mkurugenzi Mwesilage alisema kuwa Tafiti zinaonaonesha kuwa Tanzania hupokea wagonjwa wapya 42,046 kila Mwaka.

Aliongeza kuwa katika takwimu zinazo ongoza nipamoja saratani shingo ya kizazi ,saratani ya matiti,njia  ya chakula kooni.

0/Post a Comment/Comments