WADAU WA MAJI ZAIDI YA MATAIFA 30 AFRIKA WAJENGEWA UWEZO WA KUZIPIGANIA HAKI ZA MAJI.

Mratibu wa Kimataifa wa Mashahidi wa Maji Dr Nick Hepworth akizungumza wakati akitoa mafunzo kwenye warsha Maalum ya siku mbili ambayo imefanyika kuanzia Mei 11 hadi 12 Mwaka huu Jijini Adidis Ababa nchini Ethiopia.
Mwenyekiti wa Bodi Taasisi ya Shahidi wa Maji Tanzania Mhandisi Herbert Kashililah akiwaeleza Washiriki Mipango mikakati ya kufanya katika utetezi wa Rasilimali za Maji katika warsha Maalum ya siku mbili ambayo imefanyika kuanzia Mei 11 hadi 12 Mwaka huu Jijini Adidis Ababa nchini Ethiopia.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mashahidi wa Maji nchini Tanzania Abel Dugange (kulia) akiwa Pamoja na Meneja Program kutoka Shirika la Shahidi wa Maji Pendo Yera (kushoto) wakieleza na kuonyesha Kwa mfano mpango Mkakati wa moja ya Kampuni inayosababisha changamoto kwa jamii katika warsha Maalum ya siku mbili ambayo imefanyika kuanzia Mei 11 hadi 12 Mwaka huu Jijini Adidis Ababa nchini Ethiopia.
Washiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia Kwa makini mafunzo kuhusu kuzipigania haki za maji katika warsha Maalum ya siku mbili ambayo imefanyika kuanzia Mei 11 hadi 12 Mwaka huu Jijini Adidis Ababa nchini Ethiopia.
Picha ya pamoja ya wadau washiriki katika warsha Maalum ya siku mbili ambayo imefanyika kuanzia Mei 11 hadi 12 Mwaka huu Jijini Adidis Ababa nchini Ethiopia.
.........................

NA MUSSA KHALID ADDIS ABABA

Wadau mbalimbali wa Masuala ya Maji takribani 30 wakiwemo Waandishi wa Habari Barani Afrika wametakiwa kuweka kipaumbele katika kuzipigania haki za maji na maendeleo shirikishi kupitia matumizi endelevu ya Masuala ya Maji Ili kuweza kupata suluhisho la changamoto zake.

Hayo yameelezwa jijini Addis Ababa nchini Ethiopia na Mratibu wa Kimataifa wa Mashahidi wa Maji Dr Nick Hepworth wakati akizungumza kwenye warsha Maalum ya siku mbili ambayo imeanza Mei 11-12 Mwaka huu ambapo imewakutanisha waandishi wa habari,  wadau wa Masuala ya maji kutoka Mataifa mbalimbali Afrika yakiwemo Mataifa ya Tanzania Nigeria,Kenya,Zimbabwe,Ethiopia,Liberia Afrika ya Kusini ,Zambia,Malawi,Madagascar,Tunisia na Cameroon.

Akizungumza wakati akiwasilisha mada  kuhusu Mapambano ya usalama wa pamoja wa maji na jukumu la nyayo za haki za maji Dr Nick amesema kuwa Warsha hiyo ni muhimu kwani itasaidia washiriki kuongeza uelewa katika kupata haki ya maji na usawa na yanayostahimili hali ya hewa  katika sekta za ukuaji  wa Rasilimali za Maji na uchumi barani Afrika.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Kampeni na Mawasiliano
Shahidi wa Maji Kimataifa  Lexi Parfitt amesema kuwa dhamira ya kufanya Warsha hiyo ni kuwaongezea uelewa wadau hao kufahamu namna gani ya kukabiliana na changamoto za maji Ili kuleta matokeo chanya katika Jamii.

Aidha Lexi amesema kuwa Mafunzo kama hayo kwa wadau mbalimbali yakiwemo mashirika ya kiraia, vyombo vya habari na watafiti kuhusu  uchunguzi, utetezi, na hatua ya kupachika usimamizi wa maji katika sekta muhimu za kimkakati yatakuwa ni endelevu kwani dhamira yao nikuhakikisha Jamii inakuwa na uelewa wa namna ya kuzitetea na kuzilinda rasilimali za maji.

Naye Mwenyekiti wa Bodi Taasisi ya Shahidi wa Maji Tanzania Mhandisi Herbert Kashililah amewasisitiza washiriki hususani wanahabari kuyazingatia Mafunzo waliyopatiwa ikiwa ni pamoja na kufanya uchunguzi katika changamoto ya kuharibiwa rasilimali za maji.

Mshiriki wa Mafunzo hayo Enock Kimita Afisa Mkuu wa Rasilimali za Maji nchini Kenya amesema katika Mafunzo hayo ameongeza utaalamu zaidi wa kufahamu kuhusu madhara ambayo rasilimali za maji nchi za afrika zinapitia kutokana na shughuli za kibinadamu.

Amesema kuwa elimu aliyoipata hasa ya kufanya uchunguzi katika nchi ya Kenya atahakikisha anafanya jitihada za kuzilinda rasilimali za maji Kwa kufanya uchunguzi uliowakweli na wenye kuthibitika.

Naye Judith  Chepkemoi Kutoka Shirika lisilo laki serikali la SASPAD  linalohusika na kulinda rasilimali za maji amesema Mafunzo waliyoyapata yatakwenda kuwasaidia kufanya utafiti Ili kupata ushahidi wa kutosha kuhusu zile changamoto ambazo zinaikumba Miundombinu ya maji.

0/Post a Comment/Comments