Timothy Marko.
WAKALA wa Majengo nchini (TBA)imesema kufuatia maelekekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuhusiana nakuongeza muda wa Manunuzi kwa waakazi wa Magomeni wanyumba zilizopo Magomeni kota ,taasisi hiyo imeongeza muda wa Manunuzi wanyumba hizo kutoka miaka 15 iliyoekekezwa na serikali awali hadi kufikia miaka 30 huku ijumuisha miaka 5ya kukaa bure.
Akizungumza na waandishi Habari jijini Dar es salaam Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Mhandisi majengoDaudi Kondoro amesema baadaya taasisi hiyo kufanya tathmini kwakuzingatia Maelekezo ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan gharamaza ununuzi wa nyumba za Magomeni kota nishilingi Milioni 48,522,913.00 kwa nyumba ya chumba kimoja Milioni56,893,455 kwa nyumba ya vyumba viwili kwa Muda miaka 15 ya ununuzi ikijumuisha miaka mitano ya kukaa bure.
"Utaratibu wa Mauzo ya Nyumba za Magomeni kota utakuwa kwa Nyumba ya Chumba kimoja inauzwa shilingi 48,522,913 kwa malipo miaka 30 wakati Nyumba vyumba viwili inauzwa 56,893,455.00 kwamuda wa mika 30".Alisema Msanifu Daudi Kondoro.
Msanifu Kondoro alisema kuwa kufuatia barua za wakaazi 644 wakala wa majengo imeanza kuweka utaratibu wa Manunuzi wa nyumba hizo.
Alisema wakala wamajengo (TBA)imeweka utaratibu kwa wasioweza kutekeleza utaratibu huo ambao watarusiwa kukaa bure kwamiaka mitano baadamuda huo Nyumba zitalejeshwa kwa wakala wa majengo.
"Jukumu la wakala wamajengo Tanzania kuweka usimamizi wa Viwanja,Ardhi yaliyotengwa kwa matumizi ya Serikali ".aliongeza Msanifu wa majengo wa taasisi hiyo Daudi Kondoro.

Post a Comment