WATANZANIA WATAKIWA KUWEKEZA KWENYE MITI YA MATUNDA


 ..............................

Wananchi wametakiwa kwendana na kasi ya Maendeleo makubwa yanayofanywa na Raisi wa awamu ya sita Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kushiriki katika Kazi za kizalendo na kujitolea katika ulinzi wa mazingira ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi kupitia uwekezaji kilimo cha miti ya matunda

Hayo yamesemwa na Balozi wa kujitolea wa mazingira nchini Moses Mwakibolwa wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Es Salaam wakati wa zoezi la upandaji miti ya matunda Mbweni JKT. Mwakibolwa amesema wananchi wakiwekeza kwenye miti kama mradi endelevu kuna faida nyingi ikiwa ni pamoja na hewa safi, kimvuli, biashara ya matunda, pamoja na kuboresha ikolojia iliyopo "nayoa rai kwa vijana kuwekeza katika kuanzisha vitalu au bustani za matunda, kuanzisha bustani hakuhitaji eneo kubwa kwa kuwa miche iliyopo ni ya kisasa na hutoa matunda mengi kwa muda mfupi, endeleeni kuwekeza katika kukuza uchumi wa vikundi au mtu mmoja mmoja na kuepuka lawama kwa kukaa vijiweni kupoteza muda" alisema

Akizungumzia upatikanaji wa miche Mwakibolwa amesema TFS wanagawa miche bure pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kwa kushirikiana na maafisa waliopo kwenye Halmashauri na mitaa hivyo amewataka wale wenye nia kujitokeza kwenye ofisi za mitaa ili kujipatia miti mizuri ya matunda na vivuli

Aidha, amesema kampeni ya MBWENI YA KIJANI NA MAMA SAMIA itasaidia kuongeza hamasa kubwa iliyopo kwa wakazi wa Mbweni na kata za Jirani kuweza kuiga shughuli za uoteshaji miti unaofanywa na wakazi wa Malindi Estate kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali

Naye Clement Mshana Mwenyekiti wa Mtaa wa Malindi Estate amesema tatizo la mifugo linarudisha nyuma jitihada zinazofanyika na jamii kupanda miti kwani mbuzi na ng'ombe huzagaa na kuharibu miti licha ya uwepo wa sheria ndogo na kuhatarisha jitihada zinazofanyika

0/Post a Comment/Comments