Kadinali wa pili wa kanisa la Ngurumo ya upako akiongea na waandishi wa habari
Balozi Sekela Ntondolo wa kanisa la Ngurumo ya upako akiongea na waandishi wa habari wakati wa kumtumikia tuzo ya heshima Nabiii mkuu Dkt Geordavie.
Nabii mkuu Dkt Geordavie akiwa ameshikilia tuzo ya heshima aliyotunukiwa na waumini wa kanisa la Ngurumo ya upako analolichunga.
Balozi Sekela Ntondolo wa kanisa la Ngurumo ya upako akiongea na waandishi wa habari wakati wa kumtumikia tuzo ya heshima Nabiii mkuu Dkt Geordavie.
Nabii mkuu Dkt Geordavie akiwa ameshikilia tuzo ya heshima aliyotunukiwa na waumini wa kanisa la Ngurumo ya upako analolichunga.
***********
Na Richard Mrusha Arusha
Kadinali wa pili wa kanisa la Ngurumo ya upako linalochungwa na Nabii mkuu Dkt Geordavie jijini Arusha, Elizaberth Humphrey amemshukuru MUNGU kwa jambo kubwa lililofanyika leo katika kanisa hilo kwa kumpa tuzo Nabii mkuu Dkt Geordavie.
Amesema tangu walipofika mahali hapo amefanyika kuwa baraka kwao kwasababubu amekuwa mtu mwenye matendo yenye kugusa mioyo ya watu wengi
Amesema kuwa amekuwa baba mwema kwa watu wote bila kujali kabila wala dini ndio maana leo watoto wake mbele za MUNGU kwetu sisi wote
Amesema alitutoa kwenye matatizo mengi ikiwemo kuanguka kiuchumi lakini kila tulipomsogelea kwa upako ambao MUNGU ameweka ndani yake na yale mafuta ya kimungu tunazidi kufunguliwa na kuwa huru",amesema Elizaberth.
Ameongeza kuwa hiyo ndiyo sababu imewafanya leo kuwa na sherehe ya kumtunza baba yao wa kiroho Mhe, Nabii mkuu Dkt. Geordavie balozi wa amani.
Ameongeza kuwa hiyo tuzo imetengenezwa nchini china na imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu sana kama mnavyoona muonekano wake ndani yake ina moyo wa dhahabu safi pia ina ishara ya tufe maana yake dunia nzima inatambua umuhimu wake na gharama yake imeharimu kiasi cha fedha za kitanzania sh milioni kumi.
Na kwa upande wake balozi wa kanisa hilo Sekela Ntondolo amesema siku ya leo imekuwa siku nzuri sana kwao kwasababu walikuwa wanamkubidhi baba yao wa kiroho Nabiii mkuu Dkt Geordavie tuzo ya heshima
Amesema wamefanya kwasababubu ya kutambua umuhimu wake hivyo wasingeweza kuona anapewa tuzo na watu wengine ambapo wao wamejisikia fahari sana kwakuonyesha kwamba Nabiii mkuu Dkt Geordavie anafanya kazi kubwa anayoifanya kwenye maisha yao.
Ameongeza kuwa wengi walifika hapo wakiwa wamefungwa kichumi na nguvu za giza maisha ni mabaya na hukuna tumaini mahali popote lakini zaidi ya hilo walifunguliwa katika vifungo hivyo napia amewabariki.
Amesema mfano yeye mwenyewe ni mubarikiwa ambaye ameweza kubarikiwa magari kwahiyo baba yao ni mtu ambaye anagusa maisha ya watu kiroho na kimwili na nyie ni mashahidi jinsi ambavyo anawabariki watu wengi kiuchumi pikipiki za miguu mitatu (Bajaji) mitaji magari na heshima.
Ameongeza kuwa Nabii mkuu amekuwa ni mtumishi wa tofauti kabisa na ameleta sura mpya kwa kanisa la Tanzania kwa kupitia hilo ndilo lililopelekea na sisi kutambua kazi yake na kuweza kumpa tuzo ya heshima tunasikia furaha sana kupokea tuzo yetu
Mwisho.



Post a Comment