*********
Mkuu
wa wilaya ya Kwimba jijini Mwanza Ng'wilabuzu Ludigija amewataka Wazazi na walezi kuhakikisha wanahudhuria kliniki ili watoto wao waweze kupatiwa chanjo ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali pamoja na kupatiwa ushauri wa Masuala muhimu ikiwemo Lishe Bora
Ludigija ametoa maelekezo hayo wakati akizindua zahanatia ya Nyamatala iliyopo Kata Ngulla Wilaya Kwamba jijini Mwanza ambapo ametumia nafasi hiyo pia kuwasihi Wazazi na walezi kuhakikisha wanalala kwenye chandarua chenye dawa ili kujikinga na ugonjwa wa malaria
Ludigija amesema serikali itaendelea kutoa vyandarua Kwa wakazi wa wilaya hiyo na kuwasihi wakazi hao kutosubiri vyandarua vinavyotolewa na serikali huku akiwataka kufanya usafi kwenye Maeneo yao ili kuuwa mazalia ya mbu
Katika halfa ya uzinduzi wa Zahanatia ya Nyamatala Kata ya Ngulla Wilayani Kwimba jijini Mwanza wakazi wa wilaya hiyo wameshukuru Kwa hatua ya kuzinduliwa Kwa zahahati hiyo kwasababu sasa watakuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu karibu na maeneo yao
Katika hatua nyingine Ludigija amewataka Wazazi na walezi wilaya ya Kwimba kuhakikisha wanawapeleka watoro wao kupata Elimu kwakuwa ni haki yao ya msingi badala ya kukatisha masomo yao Kwa sababu mbalimbali zisizokubalika



Post a Comment