......................
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewataka wananchi kulinda miradi ya maendeleo, hifadhi ya mazingira kwa kupanda miti pamoja na kulinda uoto wa asili ili iendelee kudumu.
Dkt. Jafo amezindua miradi hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 520 ikiwemo
uchimbaji wa visima viwili virefu vya maji inayojumuisha mfumo wa sola kwa
ajili ya kuvuta maji, matanki ya kuhifadhi maji pamoja na mfumo wa umwagiliaji
na wa matumizi ya wananchi, lambo la lenye uwezo wa kukusanya maji lita za ujazo
252,299 zikiweza kumwagilia hekta 287 za mazao ya mbogamboga, kiwanda kidogo cha sabuni na kikundi cha uzalishaji uyoga.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vilivyonufaika na
mradi vya Melela, Magali na Mingo, amesema kuwa Serikali ina nia ya dhati ya
kuhakikisha wananchi katika maeneo yenye ukame wanapata mafanikio.
Amesema Serikali inapeleka miradi kwa wananchi ili kuwasaidia katika
kupata fursa za kimaendeleo pamoja licha ya kuwepo kwa changamoto za mabadiliko
ya tabiachi zinazochangia ukame.
“Ndugu zangu niwashukuru sana kwa kutekeleza hii miradi na niwaombe
tuilinde asitokee mharibifu akaja kuharibu miundombinu tumsimfumbie macho,
lakini pia ajenda yetu kuu tutunze mazingira, usipoyatunza na kuyashughulikia
mazingira yatakushughulikia”, amesisitiza.
Kutokana na hali
hiyo hivyo, Dkt. Jafo amewapongeza viongozi katika wilaya hiyo kwa usimamizi
mzuri wa miradi na kuwa wananchi wanaponufaika nayo ni jambo jambo la heri.
Kwa upande wake Mkuu
wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli amemshukuru Waziri Jafo kwa kutembelea
wilaya hiyo na kuzindua miradi hiyo kwa manufaa ya wananchi.
Mkuu wa wilaya huyo
ameahidi kwa kushirikiana na timu yake kuisimamia na kuilinda miradi hiyo ya maendeleo
kwa nguvu zote kuhakikisha inakwenda kwa wananchi kama ambavyo Serikali
inaagiza.
Aidha, Mhe. Judith amesema
wilaya yake inatekeleza shughuli za hifadhi ya mazingira ili kukabiliana na
changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa kuhakikisha inatoa elimu kwa wananchi
kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira.
Baadhi ya wananchi wakiwemo Bw. Fortunata Mathias, Said Salum na Mohamed
Seif Diwani wa Kata ya wameishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa
kuwapelekea Mradi wa EBARR.
Wsmesema kuwa kupitia mradi wa vitalu nyumba vilivyozinduliwa wataweza kujihusisha
na kilimo cha mbogamboga hivyo kujipatia kipato tofauti na hao awali amapo
walishindwa kufanya shughuli za kilimo wakati wa kiangazi.
“Sisi wa wakulima tuliteseka sana kutokana na shida ya maji iliyosababishwa
na ukame lakini sasa hivi tunafanya kazi vizuri tunamwagilia mazao yetu,
tunaomba Serikali iongeze mabwawa ili tuweza kulima Zaidi,” amesema.
Mradi
wa EBARR unatekelezwa pia katika Wilaya ya Simanjiro (Manyara), Mvomero
(Morogoro), Kishapu (Shinyanga) na Kaskazini ‘A’ Unguja (Zanzibar) chini ya
ufadhili wa Mfuko wa Mazingira wa Dunia chini ya Shirika la Mazingira la Umoja
wa Mataifa (UNEP)

.jpg)
Post a Comment