WAZIRI MKUU KUKUTANA NA WAFANYABISHARA KARIAKOO JUMATANO


 ********

Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kukutana na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo kesho Jumatano Mei 17, 2023. 

Katika mkutano huo Waziri Mkuu Majaliwa atakutana pia na mawaziri wa sekta hiyo pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Saa 8 mchana  kwenye ofisi ya Waziri Mkuu Magogoni-Ikulu na kuratibiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala.

Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri Mkuu, amewasihi wafanyabiashara wa soko hilo kuendelea na shughuli zao za biashara wakati Serikali inajiandaa kukutana nao kwa lengo la kuwasikiliza na kushughulikia kero zinazowakabili.

0/Post a Comment/Comments