Na Brown Jonas, WUSM Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu Mei 16, 2023 Mtumba jijini Dodoma, ameongoza kikao kati ya Wizara yake na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambayo imewakilishwa na RADM Michael Mumanga kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Faraji Mnyepe.
Lengo la kikao hicho ni kuwa na mpango wa pamoja ya uhifadhi na uendelezaji wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika.
Kikao hicho pia kimejadili namna ya kuendeleza ushirikiano katika wajibu wa Urithi wa Ukombozi wa Afrika ambao Tanzania ndio mwenyekiti wa Kamati ya Urithi wa Bara la Afrika.
Aidha, kikao pia kimehudhuriwa na Mratibu wa Kituo cha Ukombozi wa Bara la Afrika Boniface Kadili, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt. Julieth Kabyemela na Kaimu Mkurugenzi Sera ya Mipango Bw. Abel Shirima pamoja na baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa.




Post a Comment