BALOZI wa Hiari wa kutangaza utalii wa Kusini mwa Tanzania ,Nicholas Reynolds maarufa kama Bongozozo amesema ameweza kufanya ziara katika vivutio na kuchukua video alizosambaza katika mitandao ya kijamii ili kuvutia wataali wa nje ya nchi.
Bongozozo alifanya ziara kwa siku 13 kuanzia Juni 12 hadi 24,2023 katika mikoa ya kusini lengo nikiwa ni kutangaza utalii kwa ukanda huo.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam,na waandishi wa habari Bongozozo amesema katika ziara hiyo ameweza kurekodi video katika maeneo mbalimbali ili kusambaza katika akaunti zake za mitandao ya kijamii ikiwemo Tiktok ambayo ipo kwa lugha ya kiingereza na kufanya watu wengi kufahamu kuhusu vivutio hivyo.
Kwa upande wake mkurugenzi Mkuu wa TTB ,Damasi Mfugale amesema lengo la ziara hiyo ya mafunzo ni kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana kusini mwa Tanzania ili kuongeza ufahamu na kuongeza idadi ya watalii.
Vivutio vilivyotembelewa ni pamoja na Hifadhi za Taifa za Milima Udzungwa,Ruaha na Nyerere,pori la akiba la Mpanga Kipengere,kikundi cha Utalii wa Kitamaduni –Mtera Izazi na Hifadhi ya Urithi wa Utamaduni wa Dunia Mgofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara.

Post a Comment