NA MUSSA KHALID
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya-DCEA kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi imefanikiwa kukamata Dawa za Kulevya aina ya Heroin Kilogram 200.5 sambamba na Bangi kavu iliyokuwa tayari kusafirishwa gunia 978 katika mikoa minne nchini.
Pia Mamlaka hiyo imekamata Bangi Mbichi gunia,5465,bangi iliyosindikwa Kilogram 1.5,Methamphetamine gramu 531.43,Heroin kete 3,878,cocaine kete 138,Mililita 3,840 za dawa tiba zenye asili ya Kulevya aina ya Pethidine Pamoja na kuteketeza ekari 1,093 za mashamba ya bangi.
Hayo yameelezwa Leo jijini Dar es salaam na Kamishna Jenerali wa DCEA Aretas James Lyimo wakati akitoa taarifa ya operesheni waliyoifanya Kwenye Mikoa ya Dar es salaam,Pwani,Kilimanjaro Pamoja na Arusha.
Aidha Kamishna Jenerali Lyimo amesema kwa kushirikiana na Bodi ya Kimataifa ya Kudhibiti Dawa za Kulevya (INCB) Mamlaka imezuia kuingia nchini jumla ya Kilogram 1,507.46 za Kemikali ambazo zingeweza kutumika kutengeneza Dawa za Kulevya.
"Ukamataji huo ulifanyika kuanzia tar 25 Machi Mwaka huu hadi tar 19 Juni Mwaka huu ambapo umehusisha watuhumiwa 109 wakiwemo raia watatu wa kigeni na baadhi ya watuhumiwa wamefikishwa mahakamani na wengine wanatarajiwa kufikishwa mahakamani taratibu za kisheria zitakapokamilika"amesema Lyimo
Lyimo amesema kuwa DCEA imejipanga kikamilifu kupambana na Biashara ya Dawa za Kulevya Huku akitoa wito Kwa wanaojihusisha na Biashara hiyo waache mara moja au wajisalimishe kabla hawajafikiwa na mkono wa sheria.
Kamishna Jenerali Huyo amewasisitiza wananchi kuhakikisha wanakuwa makini na mizigo wanayopewa kubeba au kuhifadhi pasipi kujua ndani yake Kuna nini.
"Kifungu Cha 15 Cha sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dwa za Kulevya kinaeleeza kuwa ni kosa kusafirishwa Dawa za Kulevya na Mtu yeyote akithibitika kutenda kosa Hilo atawajibishwa kisheria ikiwa ni pamoja na kifungo kisichopungua miaka 30 au kifungo Cha Maisha Gerezani"ameendelea kusisitiza Kamishna Jenerali
Pia amesema kuwa Mamlaka hiyo imeendelea kutoa elimu Juu tatizo la Dawa za Kulevya Kwa jamii lakini pia imeingia Makubaliano na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa -TAKUKURU kutumia klabu zao zilizoanzishwa kwenye shule na vyuo kutoa elimu ya tatizo la Dawa za Kulevya.
Katika Hatua ngingine Mamlaka hiyo imetoa taarifa ya kufanyika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupiga vita Dawa za Kulevya Duniani kuanzia Juni 23 hadi Juni 25 Mwaka huu Jijini Arusha Huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan yakienda na Kauli Mbili isemayo "Tuzingatie utu na kuboresha Huduma za Kinga na Tiba".

Post a Comment