HAKUNA MANUSURA WENGINE AJALI YA TRENI INDIA

                         *****

Mamlaka nchini India zimesema mapema leo kuwa, waokoaji hawajafanikiwa kuwapata watu wengine walionusurika kwenye ajali iliyohusisha treni mbili za abiria na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 280.

Mamia ya watu wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo inayotajwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea ndani ya miongo kadhaa.

Treni hizo ni Coromandel Express iliyokuwa ikisafiri kutoka Howrah, jimbo la Bengali magharibi kuelekea Chena, jimboni Tamil Nadu, na Howrah Superfast Express iliyokuwa ikisafiri kutoka Bengaluru huko Karnataka kuelekea Howrah.

Ajali hiyo iliyozua mtafaruku ilitokea usiku wa Ijumaa umbali wa kilometa 220 kusini magharibi mwa mji wa Kolkata, na kuwalazimu waokoaji kupanda juu ya mabehewa ya treni yaliyoharibiwa na ajali wakivunja milango na madirisha ili kuwaokoa watu waliokuwa ndani.

Idadi ya vifo iliongezeka usiku kucha. Miili ya watu waliofariki dunia iliyofunikwa mashuka meupe ililazwa chini karibu na njia ya reli wakati wenyeji wa eneo ilikotokea ajali na waokoaji walipokuwa wakifanya juhudi kuwasaidia walionusurika.

Wanajeshi na helikopta za jeshi la anga waliunganisha juhudi hizo. Mkurugenzi wa kitengo cha dharura na zimamoto wa jimbo la Odisha, Sudhanshu Sarangi, amesema kufikia majira ya saa nne usiku, walifanikiwa kuwaokoa watu walionusurika na baada ya hapo shughuli iliyofuata ilikuwa ya kuitoa miili ya watu waliokufa kwenye ajali hiyo.

Mamlaka nchini India zimesema mapema leo kuwa, waokoaji hawajafanikiwa kuwapata watu wengine walionusurika kwenye ajali iliyohusisha treni mbili za abiria na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 280.

Mamia ya watu wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo inayotajwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea bndani ya miongo kadhaa.

Treni hizo ni Coromandel Express iliyokuwa ikisafiri kutoka Howrah, jimbo la Bengali magharibi kuelekea Chena, jimboni Tamil Nadu, na Howrah Superfast Express iliyokuwa ikisafiri kutoka Bengaluru huko Karnataka kuelekea Howrah.

Ajali hiyo iliyozua mtafaruku ilitokea usiku wa Ijumaa umbali wa kilometa 220 kusini magharibi mwa mji wa Kolkata, na kuwalazimu waokoaji kupanda juu ya mabehewa ya treni yaliyoharibiwa na ajali wakivunja milango na madirisha ili kuwaokoa watu waliokuwa ndani.

Idadi ya vifo iliongezeka usiku kucha. Miili ya watu waliofariki dunia iliyofunikwa mashuka meupe ililazwa chini karibu na njia ya reli wakati wenyeji wa eneo ilikotokea ajali na waokoaji walipokuwa wakifanya juhudi kuwasaidia walionusurika.

Juhudi za uokoaji baada ya kutokea kwa ajali ya treni IndiaJuhudi za uokoaji baada ya kutokea kwa ajali ya treni India
Juhudi za uokoaji baada ya kutokea kwa ajali ya treni IndiaPicha: Press Trust of India/dpa/picture alliance
Wanajeshi na helikopta za jeshi la anga waliunganisha juhudi hizo. Mkurugenzi wa kitengo cha dharura na zimamoto wa jimbo la Odisha, Sudhanshu Sarangi, amesema kufikia majira ya saa nne usiku, walifanikiwa kuwaokoa watu walionusurika na baada ya hapo shughuli iliyofuata ilikuwa ya kuitoa miili ya watu waliokufa kwenye ajali hiyo.

Juhudi za uokoaji usiku kucha
Takribani miili 280 ilipatikana Ijumaa usiku hadi Jumamosi asubuhi. Idadi ya majeruhi inatajwa kufikia watu 900 wakati uchunguzi wa chanzo hasa cha ajali hiyo ukiendelea. Kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa India P.K Jena, kati ya majeruhi hao, waliojeruhiwa vibaya ni 200 na wengine 200 waliruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupatiwa matibabu. Raia wengi walijitokeza kutoa damu ili kuyanusuru maisha ya majeruhi.

Hata hivyo, Jena amesema wakati shughuli za uokoaji zikielekea ukingoni, moja ya changamoto kubwa hivi sasa ni kuitambua miili ya waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo. Ameeleza kwamba, ndugu wa marehemu watapatiwa miili ya ndugu zao pale watakapofanikiwa kuthibitisha kwa Ushahidi uhusiano wao na baada ya miili kufanyiwa uchunguzi. Amesema, huenda vipimo vya vinasaba, DNA vikatumika ili kufanya utambuzi.

#Dwkiswahili

0/Post a Comment/Comments