Dar-es-Salaam
Infinix
Tanzania yazindua matoleo mapya katika series ya NOTE 30, uzinduzi wa Infinix NOTE 30, NOTE 30 PRO na NOTE 30 VIP
ambao ulifanyika mwishoni mwa wiki, Infinix imeweka rekodi mpya ya uchezaji
games na utendakazi kwa ufanisi kupitia matoleo hayo.
Kwa
kichakataji chake cha Dimensity 8050 5G,
NOTE 30 Vip 5G ina matumizi bora ya nishati, ikiruhusu kasi ya kuchakata haraka
na kufanya kazi nyingi kwa urahisi zaidi. Zaidi ya hayo, Chaji ya Haraka ya(All-Round Fast Charge) 68W na Chaji
isiyotumia waya ya(wireless charge) 50W
huhakikisha kwamba watumiaji wanaweza kuchaji simu haraka wanapocheza bila
wasiwasi wa kuongezeka kwa joto. NOTE 30 Vip 5G pia ina onyesho(refresh rate)
maridadi la 120Hz FHD+ na kamera
yenye nguvu ya 108MP iliyo na
vipengele vilivyoboreshwa kwa matumizi mazuri ya upigaji picha.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi Bw.Francis Tu alisema, “Infinix ni
brand inayotambulika duniani kote, leo tuna furaha kutangaza Infinix NOTE 30
Series, tumebuni series hii ya NOTE kwa lengo la kuwapa watumiaji simu yenye
nguvu inayoweza kuwafanya waunganishwe na ulimwengu, wakati wowote na mahali
popote.
Ili kufanikisha hili, tulitengeneza suluhisho la kwanza kwa kuvumbua
teknolojia ya ‘All-Round Fast Charge’,
ambalo sio tu linatoa kasi lakini pia huhakikisha usalama, umaridadi na umahiri.
Kwa suluhisho hili, watumiaji wanaweza kudhibiti maisha yao katika hali
zote, 24/7.
Vifaa vyote vina onyesho bora zaidi, kamera iliyo wazi kabisa, mfumo wa
sauti uliosanifiwa na JBL na uwezo
wa hali ya juu wa muunganisho.
Tuna uhakika kwamba Matoleo ya NOTE 30 ni chaguo bora kwa watumiaji wenye kutumia simu zao kama kitenda kazi kikubwa katika pirikapirika za kila siku.”
Msanii mahiri wa Bongo flavour Mario ambaye pia ni balozi wa Infinix NOTE
30 aliongelea uzoefu aliokuwa nao juu ya bidhaa hii,
“Ninahisi kuunganishwa na hii simu nikiwa kama kijana mwenye kazi nyingi za
kufanya pasipo kupoteza muda, Infinix NOTE Series imekuwa suluhisho kwangu kwa
pande zote, fikiria inachukua dakika 30 tu nishati ya betri kufikia 80%, lakini
pia inaniruhusu kucheza michezo wakati simu ikiendelea kujaa chaji, kuchajisha
simu nyengine, licha ya kuwa na sifa hizi zote zaidi ninavutiwa na gharama yake
ni rahisi kila kijana anaweza kukifikia na kutimiza malengo yake kupitia
teknolojia”.
lakini pia Mario amewataka vijana
kukaa karibu na social media page za @infinixmobiletz,
kampuni inayomjali na kumthamini kijana mwenye kipaji hivyo kumeandaliwa shindano la Star Alliance ambalo linatarajiwa kuanza hivi punde ni wakati wako kijana kutoboa kupitia kipaji chako.
Hafla hiyo ilifanyika Serena Hotel hoteli ya hadhi ya nyota 5 na kuhudhuriwa na wafanyabiashara wa simu, wafanyakazi wa kampuni za mitandao ya simu, Balozi wa NOTE 30 Bwana Mario, wateja wa simu za Infinix na medias mbalimbali. Zawadi mbalimbali zikiwamo NOTE 30 ziligawiwa kwa maduka bora na wageni waalikwa walioshinda bahati nasibu.
Infinix NOTE 30 zinapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania, au piga 0745170222 kwa huduma ya haraka.
Post a Comment