JESHI LAWATAKA WANANCHI KUSHEREKEA IDD ALHAJI KWA AMANI


 ..........................

Timothy Marko

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewataka wananchi kujiepusha na vitendo vya uhalifu kwenye kusherekea sikukuu ya Idd alhaji inayotarajia kufanyika kesho.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kamishna wa kanda Maalum wa polisi wa Dares Salaam  CP Murilo Jumanne Murilo amesema kuwa ni vyema watumiaji wavyombo vya moto kutumia vyombo hivyo kwakuzingatia sheria za usalama Barabarani.

"Tukihisi Dereva  uendeshaji wake sio mzuri Barabarani tutamkamata na kumuhoji nakisha kumpeleka mahakamani".Alisema CP Murilo Jumanne Murilo .

Kamishina wa polisi Murilo alisema wamejipanga kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yote yenyemkusanyiko wa watu kesho ikudhibiti vitendo vya kihalifu.

"Kumekuwa natabia ya vishandu kupora mikoba simu Jeshi la polisi halitosita kuwakamata watu hawa".Aliongeza Kamishina Murilo.

0/Post a Comment/Comments