MIRACLE EXPERIENCE YAJA NA HUDUMA YA UTALII CHINI YA BAHARI 'SUBMARINE TOUR'



                    *******


Na Richard Mrusha Arusha 

KAMPUNI ya Utalii ya Miracle Experience  inatarajia kuanza huduma mpya ya Utalii wa chini ya maji "Submarine Tour" ambao wageni watapata fursa ya kushuhudia mandhari ya bahari.

Akizungumza na  mwandishi wa  habari katika maonyesho ya Nne ya Utalii ya Karibu Kill Fair, Afisa masoko na biashara wa kampuni hiyo upande wa Submarine, Amani Adam amesema wanatarajia kuzindua huduma hiyo ya kipekee ndani ya visiwa vya Zanzibari, itakuwa inabeba watu 10, kwa mzunguko wa saa moja na nusu, masaa mawili  na masaa matatu.

"Huduma hii itazinduliwa rasmi Julai 15,2023 mjini Unguja, Zanzibar.

Huduma hiyo itakuwa inafanyika kila muda maalum wageni watakuwa wanatembea baharini na kutalii chini ya bahari.

Hii ni huduma ya kipekee na mara ya kwanza inafanyika Tanzania tukiwa watu wa kwanza kufanya Utalii huu kwa wageni" amesema Amani Adam.

Aidha, amesema kuwa, huduma hii ni Utalii wa kipekee ndani bahari ambapo wageni watapata fursa ya kuzama baharini na kuona vitu ndani ya bahari.

"Utalii huu wa kipekee ambao mgeni anaweza kuona vitu chini ya maji pia ni muhimu kwani utawasaidia watu wote ikiwemo walemavu ambao wangeshindwa kufanya shughuli za kuzamia 'dive' hivyo itakuwa ni ya kipekee." Amesema Amani Adam.

Utalii huo wa Submarine Experience utaendelea kutoa fursa ya ajira ikiwemo suala la kuongeza soko la utalii nchini.

Mwisho.

0/Post a Comment/Comments