********
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, *Daud Yassin* amekutana na kufanya mazungumzo na SHEIKH WA MKOA WA IRINGA, *SHEIKH SAID ABRI.*
Ziara hiyo aliyoifanya leo Jumi 29, 2023 ni mwendelezo wa utaratibu wake wa kuwatembelea viongozi wa taasisi mbalimbali na madhehebu ya Dini.
Pamoja na kumtakia EID MUBARAK, Yassin amemweleza *Sheikh Abri* kwamba Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa, kinathamini na kutambua shughuli zote zinazofanywa na VIONGOZI wa madhehebu ya DINI.
Amesema CCM Mkoa wa Iringa ipo tayari kushirikiana na kupokea ushauri kutoka kwa viongozi wa madhehebu ya DINI.
Naye Sheikh wa Mkoa wa Iringa,
*Sheikh Said Abri,* amemshukuru Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Iringa kwa kumtembelea na ameahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa ajili maslahi ya wananchi wa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla.
*Tumaini Msowoya, Iringa*
*# CCM IMARA#*
*#Kazi iendelee#*

Post a Comment