Na
Mroki Mroki, Dodoma
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata 14 za
Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 13 Julai mwaka 2023.
Akitangaza
Uchaguzi huo mdogo jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Ramadhani Kailima amesema uchaguzi huo unafanyika baada ya kupokea
taarifa kutoka kwa waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.
Amefafanua
kuwa Waziri ametoa taarifa hiyo kwa kuzingatia matakwa ya Kifungu cha 13(1) cha
Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292.
“Kutokana
na taarifa hiyo, Tume kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya
Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, inatoa taarifa kwa Umma kuhusu
uwepo wa uchaguzi mdogo wa adiwanikatika
kata 14 za Tanzania Bara”alisema Kailima.
Kailima
amezitaja kata hizo kuwa ni Kata ya Ngoywa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya
Sikonge, Kata ya Kalola iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Uyui zote za Mkoani
Tabora na Kata Sindeni Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Kata ya Potwe
Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Kata ya Kwashemshi Halmashauri ya Wilaya ya
Korogwe na Kata ya Bosha Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga zote za Mkoa wa Tanga.
Kata
zingine ni Kata ya Mahege katika Halmashauri ya Kibiti mkoa wa Pwani, Kata ya
Bunamhala katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Kata ya Njoro
na Kalemawe katika Halmashauri ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kata ya
Mnavira katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara, Kataya Kinyika
katika Halmashauri ya Wilaya ya mkoa wa Njombe.
Kailima
ametaja Kata zingine zitakazo fanya uchaguzi ni ni Kata ya Magubike katika
Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro na Kata ya Mbede katika
Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ya mkoa wa Katavi.
Amesema
ratiba ya uchaguzi huo itaanza na utoaji wa fomu za uchaguzi kwa wagombea
kuanzia tarehe 24 hadi 30 Juni , 2023 huku uteuzi wa wagombea watakao wania
nafasi hizo ukifanyika Juni 30 mwaka
huu.
Kailima
amesema vyama vitakavyopata uteuzi vitaanza kampeni za Uchaguzi tarehe 01 hadi
12 Julai na siku ya kupiga kura itakuwa tarehe 13 Julai mwaka 2023.
“Tume inatumia nafasi hii kuvikumbusha vyama vya siasa, wagombea na wadau wote wa uchaguzi uzingatia Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Taratibu, Miongozo na maelekezo katika kipindi cha uchaguzi huu mdogo” alisema Kailima.

Post a Comment