Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amawataka Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) kuangalia namna ya kuongezeka muda wa kufanya kazi hadi kufikia saa 24 badala ya muda uliopo sasa.
Ametoa kauli hiyo jana Juni 27 wakati akizindua safari za mabasi hayo kati ya Gerezani hadi Mbagala rangi tatu ambayo imelenga kurahisisha huduma ya usafiri kwa watu wanaotaka kutembelea maonyesho ya sabasaba yanayotarajia kuanza leo June 28, 2023.
Aidha amesema hafurahishwi na malalamiko yaliyokuwapo kwa muda mrefu juu ya kuchelewa kwa mabasi hayo jambo ambalo linawafanya wananchi kusubiri kituoni kwa zaidi ya saa 1.

Post a Comment