******
Serikali kupitia ofisi ya Makamu wa Rais imesema imeendelea kuweka mazingira wezeshi ikiwemo kutunga sera mpya inayohusu usimamizi wa mazingira ambayo inatoa nafasi kuhakikisha masuala ya mazingira yanatiliwa mkazo
Akizungumza mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa huduma za sheria ofisi ya makamu wa Rais ,Muungano na Mazingira Dustan Shimbo kwenye semina ya siku moja kujadili na kuendeleza fursa zilizopo katika hewa ukaa yaani cabon amesema kuwa wananchi wasiwe na wasiwasi katika kuwekeza kwenye biashara ya cabon kwani sera zilizopo ni wezeshi.
Akizungumzia fursa zilizopo kwenye biashara ya hewa ya ukaa amesema itafungua fursa nyingi kwa wananchi wanaoishi pembeni mwa misitu hususani waishio vijijini.
Naye Mshiriki wa semina hiyo Arafat Mtui kutoka wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro amesema biashara ya hewa ya ukaa ni muhimu kutokana biashara hiyo itasaidia kupunguza uhabirifu wa misitu
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa SAGCOT Centre ambao ndiyo waandaji wa semina hiyo GEOFFEY KIRENGA amesema bado ukataji miti imekuwa changamoto ambapo utafiti unaonyesha ukataji wa miti Tanzania ni asilimia 1.2 kwa mwaka huku kiwango hicho kikiwa ni kikubwa ikilinganishwa na wastani wa ukataji wa misitu duniani ambapo ni asilimia 0.8 hivyo kuwataka wananchi kuendelea.
Biashara ya hewa ukaa itafungua fursa nyingi kwa wananchi wanaoishi pembeni mwa misitu hususani waishio vijijini.



Post a Comment