Katibu tawala mkoa wa Dar es Salaam Rehema Madenge kushoto kwake ni mwakilishi mkazi wa UNFPA Mark Brian Schreiner , wakikata utepe wa kuashiria kupokea magari hayo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila.
Magari 6 yaliyotolewa na Shirika la umoja wa mataifa linaloshuhulikia maswala ya afya ya uzazi na idadi ya watu(UNFPA),.Mganga mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Dkt Rashid Mfaume akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi magari sita.
(Picha na James Salvatory)
""""""""""""
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa kupokea msaada wa magari 6 kutoka Shirika la umoja wa mataifa linaloshuhulikia maswala ya afya ya uzazi na idadi ya watu(UNFPA), katibu tawala mkoa wa Dar es Salaam Rehema Madenge amesema kuwa pamoja na juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali bado kuna vifo vinavyotokana na uzazi hivyo kuwataka watendaji watakaotumia magari hayo kuyatunza ili yaweze kuhudumia watu wengi zaidi na kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Meneja wa programu ya afya ya uzazi wa mama na mtoto kutoka Shirika UNFPA Felister Bwana amesema magari hayo yamegharimu takriban milioni 570 za kitanzania yatarahisisha utoaji wa huduma za afya katika mikoa ya dar es salaam na dodoma kutokana na uhitaji mkubwa wa mikoa hiyo.
Naye mganga mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Dkt Rashid Mfaume amebainisha kuwa wataendelea kushirikiana na shirika la UNFPA kuhakikisha afya ya uzazi, vijana pamoja na masuala ya lishe hususa ni katika maeneo ya mijini vinaboreshwa ili kukidhi wingi wa watu katika maeneo hayo.





Post a Comment