UCHAKACHUAJI WA MBOLEA NI UKATILI – DK NGAILO

Mkurugenzi Mtendaji  wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt. Stephan Ngailo aki&^iwa katika moja ya maghala ya mbolea Mkoani Njombe Ili kujionea upatikanaji wa pembejeo hiyo muhimu kabla ya msimu.wa kilimo wa 2023/2024   kuanza.

...........................

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imesema itakuja na sheria itakayowahesabu wafanyabiashara wanaochakachua mbolea kama wahujumu uchumi.

Dkt. Ngailo ameyasema hayo juzi mkoani Rukwa akiwa katika ziara mikoaYa Nyanda za Juu Kusini kuimarisha mikakati ya usambazaji wa mbolea katika msimu ujao wa 2023/2024.

Mamlaka ya Udhibidi wa Mbolea Tanzania (TFRA) imepiga marufuku kwa mfanyabishara yeyote kufanya uchakachuaji wa mbolea.

Katika msimu wa kilimo uliopita baadhi ya wafanyabiashara walibainika kuchakachua mbolea kwa kuchanganya na mchanga jambo linaloathiri ukuaji wa mazao.

Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA, Dk Stephan Ngailo ameiambia Mwananchi, leo June 7, 2023 kuwa  wanaenda kuboresha sheria ili badala ya kulipa faini, atakayebainika kufanya kosa hilo ashtakiwe kwa kosa la uhujumu uchumi na adhabu yake iwe kifungo.

“Uchakachuaji ni ukatili na uuaji, atakayebainika kwa jinsi yeyote ile adhabu yake iwe kali na isiwe faini bali kifungo moja kwa moja,” amesema Dk Ngailo.

Kulingana na TFRA, wanaendelea kusimamia udhibiti, ukaguzi na ubora wa mbolea kuanzia ngazi ya awali kiwandani au bandarini mpaka kwa walaji wa mwisho. 

“Mwaka huu kuanzia Julai 1, 2023 wataweka wawakilishi kwenye kila mkoa kwa ajili ya kuratibu na kusimamia suala la mbolea. Niwaombe wakulima wakiona jambo lisilo la kawaida wapige simu 0733 800 200, tuachukua hatua stahiki,” amesema Dk Ngailo.

Kwa upande wao baadhi ya wakulima walisema mbolea iliyochakachuliwa imekuwa mzigo mkubwa kwao kwa sababu, wakishanunua sio rahisi kuitambua.

“Fikiria unanunua mbolea kumbe imechanganywa na mchaka, ikienda kukuzia au kupandia huoni faida yoyote ile. Hii ni hatari sana kwa ukuaji wa mazao,” amesema Joseph Kilasi, mkulima wa mahindi.

Aliishauri TFRA kuweka mkakati wa kuhakikisha wanapita kwenye magodauni ya mawakala ili wafanye ukaguzi na kuwakamata mawakala wasio waaminifu ambao kwa nia mbaya wanadidimiza kilimo

0/Post a Comment/Comments