Afisa Mtendaji Mkuu wa ATE, Bi.Suzanne Ndomba akizungumza katika Mkutano wa Majadiliano wa Masuala ya Ujuzi na Wadau wa Chama Cha Waajiri Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulamavu kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali imeanzisha program mbalimbali
ya kukuza ujuzi , ambapo Vijana wapatao 91,106 wamenufaika na mafunzo ya Uanagenzi.
Akizungumza jijini Dar es salaam Katika Mkutano wa Majadiliano wa Masuala ya Ujuzi na Wadau wa Chama Cha Waajiri Tanzania (Ate), Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira Na Wenye Ulemavu) Patrobas Katambi
Amesema Vijana wapatao 22,296 wamenufaika na mafunzo ya urasimishaji ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa elimu (RPL) na vilevile Vijana wapatao 6,300 wamenufaika na mafunzo ya uzoefu wa kazi kwa wanaohitimu vyuo vya elimu ya juu na ya kati na Vijana 2,196 wamenufaika na mafunzo ya kukuza ujuzi kwa walio makazini kwa sekta ya umma na binafsi.
Aidha amewapongeza ATE kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika masuala mbalimbali ikiwemo ya kuhamasisha Usawa wa Kijinsia katika maeneo ya kazi hasa kupitia utekelezaji wa Programu ya Mwanamke Kiongozi inayolenga kuwajengea uwezo Wanawake kushika nafasi za Juu za Uongozi.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa ATE, Bi.Suzanne Ndomba amesema kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi, Serikali imetoa fursa za mafunzo ya ujuzi wa kujiajiri kuajiriwa kwa vijana 14,542 mbalimbali kupitia mafunzo ya uanagenzi na uzoefu kazini.


Post a Comment