Kamishna
msaidizi wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara
ya Maendeleo ya Jamii,jinsia wanawake na makundi maalum Baraka Makona wakati
akizungumza na waandishi wa habari katika Mkutano mkuu wa saba wa chama cha
wanasaikolojia Tanzania (TAPA) ambao umekuwa na kauli mbiu isemayo ‘Afya ya
Akili,Ustawi wa Kisaikolojia na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050’uliofanyika leo
jijini Dar es salaam.
Rais
wa Chama cha wanasaikolojia Tanzania (TAPA) Magolanga Shagembe akizungumza na
waandishi wa habari katika Mkutano mkuu wa saba wa chama cha wanasaikolojia
Tanzania (TAPA) ambao umekuwa na kauli mbiu isemayo ‘Afya ya Akili,Ustawi wa
Kisaikolojia na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050’uliofanyika leo jijini Dar es
salaam.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika linalohusika na Malezi na Makuzi ya watoto na utoaji wa huduma
ya afya ya akili kwa jamii Tanzania-REPSSI Edwick Mapalala akiwasilisha mada katika
Mkutano mkuu wa saba wa chama cha wanasaikolojia Tanzania (TAPA) ambao umekuwa
na kauli mbiu isemayo ‘Afya ya Akili,Ustawi wa Kisaikolojia na Dira ya
Maendeleo ya Taifa 2050’uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya washiriki wa Mkutano mkuu wa saba wa chama cha wanasaikolojia Tanzania
(TAPA) ambao umekuwa na kauli mbiu isemayo ‘Afya ya Akili,Ustawi wa
Kisaikolojia na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050’uliofanyika leo jijini Dar es
salaam (picha na Mussa Khalid)NA
MUSSA KHALID
Wataalamu
wa saikolojia nchini wametakiwa kujikita kujua kwa kina chanzo cha visababisho
vya matukio ya kikatili yanayoibuka kwenye jamii ili kuweza kuepukana na
matukio hayo.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Kamishna msaidizi wa Ustawi wa Jamii
kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,jinsia
wanawake na makundi maalum Baraka Makona wakati akizungumza katika Mkutano mkuu
wa saba wa chama cha wanasaikolojia Tanzania (TAPA) ambao umekuwa na kauli mbiu
isemayo ‘Afya ya Akili,Ustawi wa Kisaikolojia na Dira ya Maendeleo ya Taifa
2050’
Makona
amesema ili kuwasaidia wananchi kufahamu namna ya kupata huduma ni vyema
wataalamu hao wasaikolojia wakawa sehemu ya serikali ili kuishauri jamii iwezekuishi katika maisha ya furaha.
‘Wananchi
wengi bado hawafahamu wapi wapate huduma mbalimbali sababu masuala yote haya
ndio yanafanya aishi kuwa na furaha hivyo kama serikali tunataka hawa wataalamu
wawe ni sehemu ya serikali katika kuhakikisha kwamba huduma hizi za kuwashauri
watu wanazifahamu”amesema Makona
Kwa
upande wake Rais wa Chama cha wanasaikolojia Tanzania (TAPA) Magolanga Shagembe
amesema kuwa malengo yao ni kuhakikisha wanasimamia elimu kwa jamii ili iweze
kutambua uwezo walio nao na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kujipatia
kipato.
Amesema
kuna umuhimu wa kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa na afya nzuri ya akili na
ustawi mzuri wa kisaikolojia na kijamii katika kuweza kufanya kazi kwa ufanisi
na hivyokupunguza maovu ambayo yanachangia kukwamisha jitihada za kuweza
kufikia malengo yaliyowekwa.
Nao
Baadhi ya Washiriki katika Mkutano huo akiwemo
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika linalohusika na Malezi na Makuzi ya watoto na
utoaji wa huduma ya afya ya akili kwa jamii Tanzania-REPSSI Edwick Mapalala,pamoja
na Msaikolojia Anti Sadaka wamesema changamoto ya watu wengi inachangiwa na
matatizo ya afya ya akili.
Mkutano huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa masuala ya saikolojia,maafisa ustawi wa jamii, wanafunzi na viongozi wa kanda.

Post a Comment