WASANII wa Muziki pamoja na Filamu Mkoa wa Njombe wamemuomba Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Chama cha Mapinduzi(UWT)Mkoa wa Njombe kuwasaidia kupaza sauti zao ili changamoto mbalimbali zinazowakabili ziweze kutatuliwa.
Hayo yamebainishwa na mmoja wa wasanii hao kwa niaba ya wasanii hao katika uzinduzi wa filamu ya 'NAFSI YANGU' ya msanii kutoka mkoani humo Happy Zephania Mwesi 'Angel Kidoti' na kuudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo msanii maarufu nchini Haji Adamu 'Baba Haji'.
Akisoma risala kwa mgeni wa uzinduzi huo ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Njombe Scolastica Kevela, mmoja wa Wasanii wa Mkoa wa Njombe John Johnson 'Kavo', amesema wanaamini kupitia kwa Mwenyekiti huyo wa UWT kilio chao kinaweza kuwafikia watu wengi.
Amesema wasanii wa Mkoa wa Njombe wameweka Mkazo mkubwa katika kuhakikisha wanatangaza kazi zao za muziki na filamu na kwamba changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni kutambulika nje ya mkoa wa Njombe kwa kutokuwa na watu wenye ushawishi ili wawashike mkono.
Amesema wao kama wasanii wa mkoani humo wanajiamini kwa kuwa na uwezo mkubwa katika sanaa mbalimbali ila kutotambulika kwao nje ya mkoa sambamba na kazi zao kutochezwa katika vituo vikubwa ndicho kitu kinachowaangusha.
"Mkoa wetu umebahatika kuwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk Pindi Chana na wengine wengi, tunaamini kupitia kwa uwepo wako Mwenyekiti wa UWT Mkoa kilio chao kitamfikia Waziri huyo" amesema Kavo
Alizungumzia hilo Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Njombe Scolastica Kevela amesema amekipokea kilio cha wasanii hao likiwemo suala la ukosefu wa vifaa vya kazi na ombi la wasanii hao kuwasaidia ili kazi zao ziweze kutambulika katika vituo vikubwa vya Radio na Televisheni.
Aidha amesema UWT Mkoa wa Njombe inatambua mchango wa wasanii wa Mkoa wa Njombe katika kufikisha ujumbe mbalimbali na kusisitiza kuwa Jumuiya hiyo itaendelea kuwashika mkono huku akiwataka kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Mwenyekiti wa UWT Taifa Marry Chatanda Julai 3 Mwaka huu.
Katika uzinduzi huo Mwenyekiti huyo wa UWT Mkoa wa Njombe alitoa Scolastica Kevela alikabidhi kiasi cha Sh 500,000 kwa msanii Angel Kidoti kama sehemu ya kumuunga mkono kwa kununua flash ya filamu aliyoizindua.
Kwa upande wake Angel pamoja na kuwapongeza wasanii wenzake kwa kujitokeza katika uzinduzi huo alimshukuru Mgeni rasmi kwa kitendo chake cha kuwaunga mkono wasanii wa Mkoa wa Njombe huku akiwataka viongozi wengine kuiga mfano wake.
Ends



Post a Comment