Waziri wa Uchumi wa Bluu na Uvuvi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Suleiman Makame akizungumza katika kongamano la pili la uchumi wa Bluu
Mkuu wa Chuo cha Bahari cha Dar es salaam Dkt Tumaini Gurumo akizungumza katika kongamano la pili la uchumi wa bluu Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Uchumi wa Bluu na Uvuvi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Suleiman Makame amewataka watanzania kuchangamkia fursa zinazotokana na sekta ya bahari ikiwemo uvuvi na usafirishaji.
Ametoa kuali hiyo katika kongamano la pili la uchumi wa bluu lililoandaliwa na chuo cha Bahari cha Dar es salaam –DMI ambapo amesema zaidi ya asilimia 70 ya bidhaa zote Duniani husafirishwa kupitia bahari.
Amesema tayari serikali imeanza mchakato wa kufanya tafiti ili kuzifikia rasilimali zilizopo chini ya bahari hivyo wananchi wanapaswa kupewa elimu kuhusu uchumi unaofungamano na sekta ya bahari na kuzichangamkia.
‘’Tunayo taasisi yetu ambayo inaongoza katika shughuli za uvui wa Bahari kuu lakini muamko bado mdogo kwa Watanzania hivyo nikuchukue fursa hii kuwahimiza kuchangamkia fursa zilizopo Bahari’’ Amesema Makame.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha Bahari cha Dar es salam –DMI, Dkt Tumaini Gurumo amekili uhaba wa wataalamu katika uchumi wa bluu ambapo ametumia fursa hiyo kuwahamasisha vijana kuchangamkia fursa hiyo.
‘’Hali ya wataalamu katika maeneo ya uchumi wa bluu bado hairidhishi ukizingatia –DMI tunategemewa katika kutoa wataalamu hasa katika eneo la usafirishaji kwa njia ya maji’’ Amebainisha Dkt Tumaini.
Captain Ernest Bupamba ni Mwenyekiti wa bodi –DMI amesema chuo hicho kimejielekeza katika maeneo ambayo bado hayana muhamko ikiwemo kufundisha vijana jinsi ya ujenzi wa meli.
Post a Comment