
Kamishna wa elimu nchini Lyabwene Mutahabwa akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 26 lililoandaliwa na Chama cha Montesori Community of Tanzania (MCT) ambalo linajadili njia za ufundishaji kwa kutumia njia ya Montessori.

Kamishna wa elimu nchini Lyabwene Mutahabwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 12, 2023 mara baada ya kufungua kongamano la 26.

Baadhi ya washiriki wa Kongamano la 26 lililoandaliwa na Chama cha Montesori Community of Tanzania (MCT) ambalo linajadili njia za ufundishaji kwa kutumia njia ya Montessori wakiwa katika kongamano hilo litakalofanyika kwa siku tano.
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
Picha za pamoja za baadhi ya washiriki wa Kongamano la 26 lililoandaliwa na Chama cha Montesori Community of Tanzania (MCT) ambalo linajadili njia za ufundishaji kwa kutumia njia ya Montessori.

Mwenyekiti wa MCT, Martha Dello akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kongamano la 26 linaloendelea kufanyika katika Ukumbi wa Msimbazi Centre.
.jpeg)
Mkurugenzi Mwendeshaji wa MCT, Sarah Kiteleja akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 12, 2023 mara baada ya kufungua kongamano la 26.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa MCT, Sarah Kiteleja akifafanua jambo kwa Kamishna wa elimu nchini Lyabwene Mutahabwa alipotembelea moja ya darasa ambalo linambinu zote za kufundishia.
Matukio mbalimbali wakati wa kongamano la 26 la Chama cha Montesori Community of Tanzania (MCT).
*****
Wazazi na walezi nchini wametakiwa kuwakuza watoto kwa misingi imara ya kimwili na akili kutengeneza Taifa bora.
Maagizo Hayo yametolewa Leo ,na Kamishina wa Elimu nchini Dkt Lyabwene Mtahabwa wakati wa kongamano la 26 la wa Montessori lililofanyika Katika ukumbi WA Msimbazi Center jijini Dar es salaam ambapo amewataka wazazi na walezi kutokuwaachia walimu pekee katika elimu ya awali na msingi ambayo ndio huanza kumjenga mtoto kiakili na Mwili .
Aidha amewaasa wazazi kuwa licha ya kuwapeleka shule watoto kupata elimu pia wawape wasaaa wa kujifunza maisha halisi ya kitanzania yatakayo wasaidia watoto uwelewa wa kutosha kuhusu Jamii Yao kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo nchini.
Hata hivyo katika kongamano hilo Mkurugenzi Mtendaji Wa Montessori Sarah Kiteleja amesema lengo la kongamano hilo ambalo hufanyika kila mwaka ni kuwajengea uwezo walezi wa vituo vya watoto na walimu,kukumbushana na kutathimini nini kifanyike kukuza watoto katika misingi iliyo imara ya tabia na akili ili kuwajengea watoto uwezo kuchanganua maswala mbalimbali Katika mazingira ya maisha ya Kila siku na makuzi Yao Kwa jumla.








Post a Comment