ATE YAHUDHURIA KIKAO CHA WADAU WA MAHAKAMA KUU

.....................

Mapema leo, Ijumaa tarehe 14 Julai 2023, Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kama mdau wa Utatu pamoja na Vyama vya Wafanyakazi , Serikali, Mahakama, Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kimehudhuria  kikao cha Wadau wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi  kilichofanyika katika ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam. 

Kikao hiki kilibeba kauli mbiu iliyosema “Umuhimu wa Utatuzi wa Migogoro ya Kazi kwa njia ya Usuluhishi katika kukuza Uchumi endelevu: Wajibu wa Mahakama na Wadau”

Akifungua kikao hicho Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Mhe. Mustapha Siyani pamoja na mambo mengine alisisitiza umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya Usuluhishi. 

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.  Patrobas Katambi, alipongeza juhudi za Mahakama katika utarudi wa migogoro na matumizi ya teknolojia ili kutoa haki kwa wakati. 

Naye, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi Dkt. Yose Mlyambina, alielezea hatua ambazo Mahakama ya Kazi imeendela kufanya hasa upande wa matumizi ya tehama katika utendaji haki na kusisitiza wadaawa wa Mahakama kutumia mfumo uliowekwa ili kuweza kupitia na kupata elimu oamoja na kuhudhuria mafunzo ambayo Mahakama imekuwa inatoa kwa wadaawa kila wiki hapo Mahakamani.

Akizungumza kwa niaba ya Waajiri, Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Bi Suzanne Ndomba Doran alieleza changamoto za Usuluhishi ikiwemo elimu na pia kusisitiza kuwa Usuluhishi wa migogoro kwa njia ya Usuluhishi  unapunguza gharama na kujenga Mahusiano. 

Sambamba na hayo Bi. Ndomba-Doran pia alieleza juhudi mbalimbali zinazofanywa na ATE ikiwemo kutoa elimu kwa Waajiri kwa kushirikiana na wadau wengine.

0/Post a Comment/Comments