AWESO-WATANZANIA TUNAPASWA KUZILINDA RASILIMALI ZA MAJI

Waziri wa Maji Jumaa Awesu (Kushoto) akiwa na Waziri wa Maji wa Malawi M Abida Sidik Mia katika mkutano wa pili wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe ambao umefayika leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Maji Jumaa Awesu akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa pili wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe ambao umefayika leo jijini Dar es salaam.

Baadhi washiriki wa mkutano wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe unaofanyika jijini Dar es Salaam.Picha ya pamoja Waziri wa Maji Tanzania na Mwenyekiti wa Mwenza wa Baraza hilo Jumaa Aweso Pamoja na Waziri wa Maji na usafi wa Mazingira  Malawi ambaye ni Mwenyekiti Mwezawa Baraza hilo Abida Audio Mia pamoja na mawaziri Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula Anthony Mavunde, Naibu Waziri wa Kilimo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato (Picha na Mussa Khalid)

.......................

NA MUSSA KHALID

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewataka watanzania Kuzilinda na kuzitunza rasilimali za maji ili kuepukana na changamoto zinazotokana na uharibifu wake.

Hayo yamejiri Leo jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Pili wa Baraza la Mawaziri wa Kamisheni ya Pamoja na Bonde la Mto Songwe ambao umewakutanisha Waziri wa Maji Tanzania na Mwenyekiti wa Mwenza wa Baraza hilo Jumaa Aweso Pamoja na Waziri wa Maji na usafi wa Mazingira  Malawi ambaye ni Mwenyekiti Mwezawa Baraza hilo Abida Audio Mia sambamba na kupitisha Bajeti ya Bonde Hilo.

Akizungumza katika Mkutano huo Waziri Jumaa Aweso amesema wananchi waendelee kuzitunza rasilimali za maji kwani hayana mbadala wake.

‘Tunakubali kwamba rasilimali za maji zimeumbwa na Mwenyezimungu lakini tusisahau wananchi kwamba tunawajibu na kutunza rasilimaji za maji kwani tumeshuhudia miaka ya nyuma kulikuwa na baadhi ya chemchem leo haipo mwaka jana jiji la Dar es salaam kwamba Mto Ruvu ambao ni chanzo kikuu cha maji kilikauka na watu walipata changamoto kubwa hivyo lile liwe funzo’amesema Waziri Aweso

 Pia Waziri aweso amesema kuwa Rasilimali za maji hazina mipaka na ndio maana hata Mto Songwe unapita mpaka nchi ya Malawi hivyo amewataka kuunganguvu ya pamoja ili kuhakikisha bonde hilo linakuwa endelevu kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.

Kwa upande wake Waziri wa Maji na usafi wa Mazingira  Malawi ambaye ni Mwenyekiti Mweza wa Baraza hilo Abida Audio Mia amesema kuwa watu wa maeneo watanufaika na mto huo katika kupata huduma mbalimbali za kijamii huku  Mkurugenzi wa Rasilimali maji Wizara ya Maji Dr George Lugomela akisema mradi ukikamilika utazuia mafuriko. 

Hivi karibuni Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Mashahidi wa maji kupitia Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Abel Dugange akizungumza wakati wa mafunzo kwa mashahidi wa maji amesema wataendelea kuwajengea uwezo kwa kushirikiana na vyombo vya habari ili kuweza kupaza sauti kwa kuzilinda na kuzitetea rasilimali za maji katika maeneo mbalimbali nchini.

Hata hivyo katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Kamisheni ya Pamoja na Bonde la Mto Songwe ambao umefanyika leo pia umewajumuisha Mawaziri wa Tanzania akiwemo Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula Anthony Mavunde, Naibu Waziri wa Kilimo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato.

0/Post a Comment/Comments