BAKWATA YASIKITISHWA NA KITENDO CHA QURANI KUCHANWA NA KUCHOMWA SWIDEN

Kaimu Mufti na Naibu Qadhi Mkuu wa Baraza hilo Shekh Ali Hamisi Ngeruko akitoa taarifa kwa waandishi wahabari jijini Dar es salaam akitolea taarifa kitendo kilichotokea katika nchi ya Sweden ya kuchanwa kwa kurasa za Quran Kisha kuchomwa moto
......................

NA MUSSA KHALID

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania-BAKWATA limesikitishwa na kitendo kilichotokea katika nchi ya Sweden ya kuchanwa kwa kurasa za Quran Kisha kuchomwa moto. 

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Kaimu Mufti na Naibu Qadhi Mkuu wa Baraza hilo Shekh Ali Hamisi Ngeruko amesema kuwa kitendo hicho hakikubaliki sio tu kwa kuwa kitabu kilichofanyiwa ni Quran Bali kitabu chochote kile kiwacho cha imani yeyote ile kufanyiwa yaliyofanyiwa kitabu hicho Huwa chachu ya moto na chuki na hasama lakini pia huwakilisha dharau na kejeli kwa waumini wa kitabu hicho.

Shekh Ngeruko amesema kuwa Baraza hilo linaitaka serikali ya Sweden kuhakikisha vitendo vya namna hiyo havitokei tena kwa lengo la kulinda hisia za waislamu ulimwenguni ikiwemo Tanzania ambayo imekuwa na uhusiano na nchi hiyo kwa miaka mingi.

Hata hivyo Baraza hilo limewasihi waislamukuwa na subira na uvumilivu katika wakati huu na kutumia nguvu na busara katika kuhamasisha na kuwahimiza wanadamu popote pale walipo waisome Qurani badala ya kuichoma na kuibeza.

0/Post a Comment/Comments