CHOKI NA BELLA KUKIWASHA NANE NANE

  

 
*********


Timothy Marko 

Katika kuhakikisha Wakaazi wa mkoa wa Mbeya wanapata burudani, Grand Gala Dance limeandaaa tamasha lakusherekea sikuu ya Nane Nane jijini Mbeya.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mratibu wa tamasha hilo Mboni Masimba amesema tamasha hilo litawajumuisha bendi za muziki ikiwemo Twanga pepeta chini ya Ally choki pamoja na Malaika bendi chini ya Christian Bella "Obama ".

"Katika tamasha hili rangi ya Vazi letu la siku hiyo ni Nyeusi na nyekundu ,ambapo Kiingilio VIP ni shilingi milioni1 kwa wakati tiketi kwa mtu moja ni shilingi 50,000".Alisema Mboni Masimba.

Mboni alisema mbali na bendi ya twanga pepeta na malaika bendi pia kutakuwa na bendi ya Msondo ngoma "baba ya Muziki".
Naye Msanii wa Muziki wa Dance kutoka Malaika Band Christian Bella "Obama " amesema kuwa bendi hiyo imejiandaa kutumbuiza katika mkesha wanane mjini Mbeya.

Bella anayetamba na Wimbo" ukowapi mpenzi" wangu anatarajia kutumbuiza usiku wa sikukuu ya nane mjini Mbeya.
"Tunakuja mbeya kwenye sikuu ya Nane nane kwenye mkesha wa kukaribisha siku  ya wakulima kwenye Gala Dance "Alisema Christian Bella. 

Naye Msanii wa Bendi ya Twanga pepeta Ally Choki mzee wa farsi amesema wanakwenda kutoa burudani kwa wakaazi wambeyakatika usiku wa kukaribisha sikuu ya wakulima.
1
"Twanga pepeta tutakuwa kwenye Gala Dance tukiangusha mojamoja na vibao kama Aminata".Alisema  Ally Choki.
Kwa upande wake  Muwakilishi wa Bendi ya Msondongoma Baba ya Muziki Rajabu Said amesema kuwa bendi yao itawanogesha wapenzi wa bendi hiyo ikiwemo  nyimbo mpya na zile za zamani.

"Bendi yetu inawasanii wakizazi cha zamani na nakizazi kipya tutawanogesha nyimbo za zamani na za sasa kwa wapenzi wetu wa muziki wa Dance "Alisema Rajabu Saidi.

0/Post a Comment/Comments