COSTECH YAASWA KUENDELEA KUKUZA NA KUIBUA BUNIFU MBALIMBALI.

.........................................

NA MUSSA KHALID

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Omary Juma Kipanga ameitaka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia –COSTECH kuendelea kukuza na kuibua bunifu mbalimbali ili kuweza kutatua matatizo ya Tanzania na Ulimwengu.

Pia amesema serikali itaendelea kusimamia kwa karibu sekta hiyo kwani imewekeza kutoka Shiling Bill 3-9 kwenye eneo la ubunifu jambo ambalo linakwenda kutafuta suluhu ya changamoto katika sekta mbalimbali.

Naibu Waziri Kipanga amesema hayo jijini Dar es salaam alipotendelea banda la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia –COSTECH katika maonyesho ya biashara ya kimataifa ya 47 yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya sabasaba mkoani Dar es Salaam.

‘Tunafahamu kwamba  katika miaka michache iliyopita bajeti yetu kwenye eneo la ubunifu Bill 3 hivyo kwa sasa kuongezeka ndio itasaidia kuendelea kukuza na kutatua changamoto kwa wazalishaji’amesema Naibu Waziri Kipanga.

 Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia –COSTECH Dkt Amosi Nungu amesema kuwa serikali hufanya uwezeshaji kwa vijana mbalimbali ili waweze kuwekeza na kukuza maendeleo ya nchi.

Aidha Naibu Waziri Kipanga amesema Wizara ya Elimu itatengeneza ushirikiano na Wizara ya Kilimo kwani vijana wengi wamekuwa wakifanya bunifu katika kilimo na hivyo kutengeneza ajira kwa wingi.

0/Post a Comment/Comments