Kamishna
Msaidizi Kinga na Huduma za Jamii Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya nchini (DCEA) Moza Makumbuli wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwenye banda lao lililopo katika viwanja
vya Maonesho ya 47 kimataifa ya biashara
Sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam.NA MUSSA KHALID
Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya nchini
(DCEA) imewataka watanzania wanaishi na waraibu wa Dawa za Kulevya katika
ameneo yao kutowanyanyapaa watu hao bali wawaelekeze kwenda kupata tiba ili waachane
na uraibu wa dawa hizo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Kamishna Msaidizi Kinga na Huduma za Jamii Moza Makumbuli wakati akizungumza na kituo hiki katika viwanja vya Maonesho ya 47 kimataifa ya biashara Sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi Makumbuli amesema kuwa DCEA
ina jukumu la kuhakikisha wanapunguza Dawa za Kulevya nchini sambamba na
kuwakinga Watanzania wasiweze kujiingiza katika matumizi ya dawa hizo.
‘Tupo hapa katika viwanja vya sabasaba katika banda la Jakaya Kikwete kwa ajili ya kutoa elimu hivyo tunawakaribisha watanzania waje kututembelea kwani watapata elimu na kuzifahamu dawa za kulevya na kuziona na kama wanachangamoto zozote watatueleza’amesema Makumbuli
Pia amesema wananchi watakapotembelea katika banda lao watapatiwa usaidizi sambamba na kuelimishwa kuhusu taasisi mbalimbali ambazo zinaweza kuwapatia msaada kama soba house.
Amesema changamoto waliyoibaini kutoka kwa wananchi wanaotembelea banda lao ni kutofahamu aina za dawa za kulevya hivyo amewataka kujitokeza kwa wingi katika banda lao ili kuweza kupata elimu hiyo.
Aidha kuhusu waraibu kunyanyapaliwa,
ameikumbusha jamii kutowanyanyapaa badala yake wawathamini ikiwa ni pamoja na
kuwasaidia namna ya kuepukana na matumizi ya dawa hizo.
Hata hivyo Makumbuli ameikumbusha jamii kutambua kuwa mapambano ya dawa za kulevya ni nguvu ya wote kwani yanaathiri watu hasa watoto hivyo kila mmoja ni vyema akawajibika sambamba na kutoa taarifa


Post a Comment