LHRC: VYOMBO VYA HAKI JINAI VITEKELEZE MAPENDEKEZO YA TUME


******
 Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC imevitaka  vyombo vinavyohusika na Haki jinai nchini vianze kutekelezeka Mapendekezo ya Tume hasa Yale yasiyohitaji matumizi ya fedha au kubadilisha sheria.

Aidha wamewataka wadau wa Haki Jinai nchini kushirikiana na serikali kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutii sheria bila shuruti ili kuepuka migogoro isyo ya lazima na vyombo vya Dola.

Akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa Mapendekezo muhimu yaliyowasilishwa na Tume ya Haki jinai kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkurugenzi Mtendaji LHRC, Anna Henga ameishauri serikali kutekeleza pendekezo la Tume la kuanzisha na kuanzishwa kwa Mamlaka mpya na huru inayojitegemea itakayojulikana kama ofisi ya Taifa ya upelelezi (OUT) itakayokuwa na Mamlaka ya kupeleleza kesi zote za jinai.

Mbali na hayo, LHRC imeiomba serikali ipeleke miswada ya sheria katika Bunge la mwezi Septemba katika Mapendekezo ambayo yanahitaji mabadiliko ya sheria

Pia LHRC imesema ni vyema kukawa na mfumo wa kufanya tathmini juu ya utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume.

Kuhusu Dhamana, Henga amependekeza kupelekwa kwa mswaada wa sheria ya Dhamana kama ilivyopendekezwa na Tume ili kutoa mwanya kwa masuala yote yanayohusu kuwa chini ya sheria Moja tofauti na sasa ambapo suala la Dhamana linaongozwa na sheria tofauti tofauti kulingana na kosa husika.

Kwa upande wa adhabu ya kifo LHRC imependekeza adhabu hiyo kufutwa.

0/Post a Comment/Comments