Mkurugenzi
Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga wakati akitoa taarifa kwa wanahabari
kuhusu kuelekea msimu wa pili wa Mwalimu Nyerere Marathon Mwaka huu
zinazotarajiwa kufanyika septemba 30 Mwaka huu.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakitekeleza majukumu yao.
......................
NA MUSSA KHALID
Makumbusho ya Taifa la Tanzania Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini,imeandaa Mbio za Mwalimu Nyerere Marathon ili kutangaza Historia ya Baba wa Taifa,kukuza utalii wa ndani itakayosaidia kujenga afya njema na kuongeza kipato kwa jamii na Mtu Mmoja Mmoja.
Hayo yameelezwa Leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga wakati akitoa taarifa kwa wanahabari kuhusu kuelekea msimu wa pili wa Mwalimu Nyerere Marathon Mwaka huu zinazotarajiwa kufanyika septemba 30 Mwaka huu.
Dkt Lwoga amesema kuwa Mwalimu Nyerere Marathon ni mwendelezo wa Program ya miaka 10 ya kuenzi na kusheherekea Urithi wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Aidha amesema kuwa kwa mwaka huu Mbio hizo zinalenga kukusanya Fedha na vifaa vya kuandaa kuweka onesho Maalum kwa ajili ya watu wenye mahitaji Maalum wasioona na wenye uono hafifu kwa kutumia matumizi ya sauti na nukta nundu.
"Kuhusu mbio Hizi tutakuwa na mbio za kilomita 22 zikiwakilisha Mwaka aliozaliwa,mbio za kilomita 13 zikiwakilisha tarehe aliyozaliwa,na mbio za kilomita 4 zikiwakilisha Mwezi aliozaliwa Baba wa Taifa"amesema Dokta Lwoga
Dkt Lwoga amesema kuwa njia kuu itakayotumika katika mbio Hizo ni pamoja na Barabara ya Butiama kwenda Busega ambayo Mwalimu Nyerere aliitumia kwenda Shule ya Msingi kila siku na kurudi Nyumbani.
Kuhusu gharama ya ushiriki Mkurugenzi Huyo wa Makumbusho ya Taifa amesema ni Shilingi 30,000/- Kwa watu wazima na wanafunzi ni Shilingi 5000 kwa Mwaka huu.
Amesema kuwa Ili kufanikisha mbio Hizo,vinahitajika na vifaa mbalimbali kama vile medali,fulana,kofia,vipeperushi,mabango,vinywaji hivyo amewaalika wadau na wafadhili kushirikiana katika kufanikisha tukio Hilo muhimu ambapo watakaochangia watapata fursa ya kutangaza huduma na bidhaa zao wakati wa maandalizi na wakati wa mbio.
"Kuhusu zawadi kwa washindi,mshindi wa kwanza wa kike na wa kiume kilomiteta 22 watapata Tsh 1,000,000 Kila Mmoja,mshindi wa pili wa kike na wa kiume watapata Tsh.750,000,mshindi wa tatu atapata 500,000 Huku mshindi wa nne 2 watapata 200,000"ameesiiatiza Dkt Lwoga

Post a Comment