Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akizungumza kwenye mkutano na wanahabari leo jijini Dar es salaam.
Rai imetolewa kwa Viongozi, Mawaziri na Wabunge kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Sababu ya jitihada zake mbalimbali anazofanya ili kuhakikisha Uchumi wa Tanzania unaimarika.
Akizungumza mapema leo,Julai 6, 2023, Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama, amesema kuwa Wabunge pamoja na viongozi wengine wanapaswa kuwa imara katika kupeperusha sera nzuri za Tanzania, na kwamba, hawapaswi kubaki nyuma katika kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais.
“Watu wote ambao wenye nia mbaya na nchi yetu, lazima tupambane nao bila kuwaogopa wala kuwaonea haya. Nchi yetu ni ya kila mtamzania, na ana haki ya kupambana kuhakikisha Amani, Utulivu na mshikamano tulionao unaendelea kuwepo.
“Rais anafanya kazi kubwa sana, mambo mengi yalikuwa hayaendi, lakini sasa mambo yanaenda vizuri sana, wawekezaji wakubwa, wadogo na wa kati wanakuja kuwekeza nchini kwetu, haya yote ni matunda yatokanayo na yeye kutembelea kwenye Nchi mbalimbali za kigeni kuunganisha Biashara ili kukuza uchumi wa nchi” amesema.

Post a Comment