MTAJI UTT AMIS WAFIKA TRIONI MOJA NA NUSU


 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uwekezaji nchini (UTT AMIS), Simon Migangala akizungumza katika kikao kazi baina ya Wahariri na taasisi hiyo kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina,


Meneja Masoko wa Taasisi ya Uwekezaji nchini (UTT AMIS),  Daudi Mbaga akizungumza katika kikao kazi baina ya Wahariri na waandishi wa habari na taasisi hiyo leo Jumatatu Julai 31, 2023. 

Mjumbe wa jukwaa la wahariri (TEF) Anjella Akilimali. 






Wahariri na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali nchini  wakiwa kweny kikao kazi na taasisi hiyo leo Jumatatu Julai 31, 2023. 
                            
(PICHA ZOTE NA JAMES SALVATORY) 
                               *******

Na Mwandishi Wetu

Imeelezwa kuwa Mtaji wa Taasisi ya Uwekezaji nchini (UTT AMIS), umeongezeka kwa kasi na kufikia Sh1.5 katika kipindi cha miaka minne.

Akizungumza leo Jumatatu Julai 31, 2023 katika kikao kazi baina ya Wahariri na taasisi hiyo kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Simon Migangala amesema ukuaji huo ni sawa na asilimia 54.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, mwaka 2009 taasisi hiyo ilianza na mtaji wa Sh65.9 bilioni na kupanda hadi kufikia Sh1.535 trioni mwaka 2023.

“Tumekuwa na ukuaji mkubwa sana. Kila Mwaka tumekuwa tunavuka malengo yetu na faida kwa wateja wetu nayo inaongezeka kila kukicha ukilinganishwa na taasisi ilipoanza,” amesisitiza Mkurugenzi wa taasisi hiyo.

Naye Meneja Masoko, Daudi Mbaga amesema kuwa taasisi hiyo inatoa mafao saba ambayo ni Umoja, Wekeza, Watoto, Jikimu, Liquid na Hatifungani.

Amesema kwa sasa wastani wa faida inayopatikana katila
Mifuko hiyo ni asilimia 12 kwa mwaka..

Kwa upande wake Mjumbe wa jukwaa la wahariri (TEF) Anjella Akilimali amesema mkutano huo na kampuni hiyo umewafanya kuyafahamu mengi hivyo watakuwa daraja la kuwafikishia wananchi elimu juu ya uwekezaji huo.

0/Post a Comment/Comments