""""""
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Atupele Mwakibete amezindua Ripoti ya Sensa ya Vyombo Vidogo vya Usafiri Majini katika eneo la Tanzania Bara, 2021.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika fanyika jana Julai 11, 2023 jijini Dar es Salaam, amelipongeza Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa kufanikisha tukio hilo la kihistoria nchini.
“Ni jambo la kwanza katika historia ya Nchi yetu, ukanda wa Afrika Mashariki na Ukanda wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kuhesabu vyombo Vidogo vya majini,” amesema Mwakibete.
Mwakibete amesema Kwamba vyombo Vidogo vya majini vina Mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Hivyo ametumia fursa hiyo kuwataka Wadau mbalimbali hususan Serikali kutumia taarifa hiyo kuboresha Sera na mipango kuhusu vyombo Vidogo vya majini na kuboresha katika matumizi ya usafiri wa majini.
Amewataka Wadau na TASAC kuitumia taarifa hiyo katika kushauri matumizi ya vyombo hivyo yanayoendana na maeneo husuka ili kuepuka na kudhibiti ajali za majini.
Kadhalika Mwakibete ameitaka TASAC na wadau kuhakikisha wanatumia taarifa hiyo katika kuboresha utendaji wao.
“Niwaombe Wadau kutumia taarifa hizi za Sensa hii kuboresha utendaji katika Sekta ya uchumi hususan uchumi wa bluu,” ameongeza Mwakibete.
Mwakibete ameongeza kushauri kuwa Ripoti hiyo isaidia katika maboresho ya shughuli za uokoaji ajali zinapotokea majini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Kaimu Mkeyenge amesema kwamba Sensa hiyo uliofanyika kwa kutembelea maeneo ya mito, maziwa, Bahari na mabwawa kwa Tanzania Bara.
Kwamba maandalizi ya Sensa hiyo yalihusisha wataalam kutoka TASAC, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Wizara ya Uvuvi na Wizara Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Hivyo amesema wameanzisha kanzidata ya vyombo hivyo na taarifa zake kwa kubainisha wamiliki, mahali vilipo, matumizi yake, nyezo zake za mawasiliano, nyenzo zake za wokozi na kadhalika.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ripoti hiyo ni kwamba idadi ya jumla ya vyombo vya majini nchini ni 52,189, idadi ya jumla ya mialo ya vyombo hivyo ni 885 na idadi ya vyombo hivyo vyenye urefu wa mita nne au zaidi ni 45,976.


Post a Comment