Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ameeleza mikakati mbalimbali inayoendelea kufanywa na Serikali ya Tanzania katika kufanikisha Tanzania kuwa na Uchumi wa kidijitali.
Ameyasema hayo leo tarehe 8 Julai, 2023 wakati akifungua rasmi siku maalum ya TEHAMA, katika Viwanja vya Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba).
Aidha wakati wa ufunguzi huo, Mhe. Nape Nnauye amezitaka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kusimamia Sera, Mikakati, Sheria na Kanuni za Mawasiliano ili kuendelea kujenga uchumi wa kidijitali nchini.
Sambamba na hilo, Mhe. Waziri amewataka wananchi kuendelea kutumia kila fursa ya TEHAMA sambamba na kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika kuboresha huduma za TEHAMA lengo hasa ikiwa ni kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa Kidijitali
Vilevile, Mhe. Waziri Nape ametumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Wizara hii yenye lengo la kurahisisha huduma za TEHAMA nchini
Ikumbukwe kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanikisha ujenzi wa miundombinu ya Anwani za Makazi pamoja na kupeleka minara zaidi ya 700 katika maeneo mbalimbali nchini, hii ni kuhakikisha sehemu nyingi nchini zinapata Mawasili


Post a Comment