Timothy Marko
MSANII wa Maigizo nchini Steve Nyerere amesema kuwa wanaobeza mkataba wa Dp world na Bandari ya Tanzania wanaagenda yao ya siri .
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Steven Nyerere amesema wanaobeza mkataba wa Dp world na Tanzania wanapambania nafasi za uongozi 2025 nakutaka watanzania kuheshimu Mamlaka iliyowekwa.
" Watanzania waondokane na kushindana na Mamlaka, Hakuna anayeshindana na Mamlaka akashinda"Alisema Steve Nyerere.
Steve Nyerere Alisema kuwa nivyema watu wamuache Rais Dk Samia Suhulu Hassani afanyekazi.
Aliongeza kuwa kumekuwa na Baadhi ya watu wamekuwa wakihongwa ili kudhohofisha juhudi za serikali kuboresha sekta ya Bandari nchini.
Katika hatua nyingine MSANII huyo katika kuboresha sekta ya Elimu
msanii huyo amezindua kusambaza mafutari nchini ilikuboresha sekta Elimu nchini.
Naye Mkurugenzi wa taasisi ya yoge Wakili Phiona Malongo taasisi hiyo imejikita kuboresha sekta ya Elimu ili kujenga kizazi bora cha badae.
Alisema Mradi huo wakusambaza madafutari nchini unalenga kugusa mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.

Post a Comment