Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura akihudumia wananchi waliotembelea banda la TAA kwenye maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
*****
Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA), imesema imeendelea kujenga Viwanja vipya na kuboresha vya zamani ili kupokea wawekezaji wanaokuja kuwekeza Nchini hali itakayosaidia kuendelea kukuza uchumi wa nchi.
Hayo yamesema na Mkurugenzi wa TAA, Mussa Mbura kwenye maonesho ya 47ya biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Kambalage Nyerere ambapo amesema kuwa mamlaka hiyo imekasimiwa na kuendesha Viwanja vya ndege vya Serikali na kuendesha na kusimamia kwa niaba ya Serikali ambayo unaendesha Viwanja 58 ambavyo vyote vipo Tanzania bara.
"Vipo Viwanja vikubwa ambavyo vimekuwa vukitumiwa sana na Serikali kusafirisha abiria kutoka ndani na nje ya Nchi, ikiwemo Kiwanja Cha Mwalimu Juliaus Kambalage Nyerere na kama mjuavyo kauli mbiu inayosema Tanzania ni mahali sahihi biashara na Uwekezaji,kwa sababu wawekezaji Hawa ili waweze kuja Nchini lazima watumie Viwanja vya ndege na ni asilimia 60 ya wageni hufika Nchi kwa kutumia Viwanja hivyo.
"Baada ya ugonjwa wa uviko 19,tunapokea wageni,wawekezaji wanaoingia Nchini na kwa kulitambua hilo Serikali yetu ya Raisi Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha Viwanja vipya na kwa sasa tuna mradi mkubwa kule msalato.
"Kufuatia filamu yetu ya. Royal Tour imefanya wageni wengi waweze kuja kwa ajili ya kuangalia vivutio mbalimbali vilivyopo Nchini kwa hiyo Viwanja vyetu viko salama pamoja na kuwa na taa ili kurahisisha wasafikiri kusafiri na kufika muda wowote," amesema Mbura.
Hivyo basi niwaombe Watanzania wote kwa ujumla wafike katika Banda letu ili waweze kupata elimu na kutangaza fursa ambazo zipo katika Viwanja vya ndege


Post a Comment