Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha wajasiliamali wanawezeshwakiuchumi,Shirika la Maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP)kwa kushirikiana na Tanzania limeanzisha mpango maalum wa kuwezesha wakulima wajasliamali kuweza kuuza mazao ya kibiashara katika kuhakikisha masoko ya bidhaa zao zinapata kufahamika kibiashara.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Meneja Miradi wa shirika la Maendeleo la umoja wa mataifa UNDP Miriam Mondosha amesema kuwa shirika hilo linaendelea kushirikiana na serikali katika kukuza Eneo huru la kibiashara. "Katika kukuza Eneo la kibiashara tutangalia nimazao gani ambayo tutaenda kuuza katika Eneo huru la kibiashara ".Alisema Mariam Mondosha.
Muwakilishi wa Shirika la Maendeleo la umoja wa mataifa UNDP Miriam Mondosha Alisema kuwa warsha hiyo inalenga kuwajengea uwezo wajasiliamali wa dogowadogo kuweza kukuza Biashara zao.
Naye Afisa Biashara Mkuu wa wizara ya viwanda na Biashara Skela Mwaisela Alisema warsha hiyo inalenga kuja nakamati litakatalojadili mkakati wa Eneo huru la kibiashara la Afrika.
"Afrika tunafanya Biashara na maeneo mengine ya kibiashara ya dunia kwa asilimia 16"Alisema sekela Mwaisela.

Post a Comment