Na.Beatrice Sanga MAELEZO
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba ametembelea Banda la Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari mara baada ya kushiriki katika mdahalo ulioandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), kuhusu Mafuta na gesi asilia uliofanyika katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba)
Katika kila maonesho ya kila mwaka TanTrade huwa wanaandaa makongamano kupitia sekta mbalimbali za serikali na Binafsi ambapo leo Julai 3, 2023 ni siku ya Mafuta na gesi asilia Katika maonesho hayo.
Mramba ameeleza kuwa Serikali inaendelea na jitihada za kuifanya nishati jadidifu kuwa nishati ya umeme ambayo ni mbadala wa mabadiliko ya hali ya hewa katika uzalishaji umeme.
"Na nyinyi mnafahamu kwamba dunia inaanza kufikiria kuhama kwenye matumizi ya nishati chafu inayozalisha gesi ya ukaa kwa wingi na kuhamia kwenye gesi safi zaidi, lakini kwa Tanzania tuna bahati kwamba sisi tuna gesi ambayo inaviwango vidogo sana vya hewa ukaa, lakini pia serikali inatazamia na ilikuwa na mazungumzo na wawekezaji kwenye eneo la mradi wa LNG na mazungumzo hayo yamefika mwisho na sasa tunaenda kupata gesi safi na ya uhakika", Mhandisi Mramba.
Mramba amesema kuwa Serikali ipo kwenye hatua ya kukamilisha mazungumzo na kikubwa katika mradi huo ni manufaa makubwa yanayotarajiwa kwa wananchi kuhusu mradi huo
Ameyataja manufaa hayo kuwa ni kuanza kunufaika na gesi ambayo imegunduliwa muda mrefu na haijaweza kutumika kwa kiasi kikubwa ambapo matumizi ya gesi hiyo mpaka sasa ni kuzalisha umeme, ambao zaidi ya asilimia 64 ya umeme unaozalishwa nchini unatokana na gesi asilia.
Ameongeza kuwa mradi wa LNG ndiyo mradi ambao utaiwezesha Tanzania kuuza gesi nje ya nchi na kunufaika kutoka katika rasilimali hiyo ambayo inapatika katika maeneo ya Mtwara na Lindi
Aidha, Mramba amesema kuwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali Serikali inaangalia katika kuzalisha umeme kupitia chanzo cha Jotoardhi ambapo katika maeneo ya Songwe, Mbeya Wilayani Tukuyu, ziwa Natroni mkoani Arusha na maeneo mengine katika Mkoa wa Pwani.
MWISHO



Post a Comment